In Summary

• Wanyonyi ndiye mgombea wa pekee anayetaka kuteuliwa na chama cha ODM kwa kiti cha gavana wa Jiji la Nairobi lakini kufikia sasa hajapokea cheti cha uteuzi.

• Wanyonyi anatazamiwa kumenyana na Johnson Sakaja wa Kenya Kwanza.

 

Catherine Mumma mwenyekiti wa bodi ya uchaguzi ya ODM
Image: HISANI

Shinikizo zazidi kutolewa kwa chama cha ODM kupeana tikiti yake ya ugavana wa Nairobi moja kwa moja kwa mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi.

Mbunge huyo wa Westlands ndiye mgombea wa pekee anayetaka kuteuliwa na chama hicho kwa kiti cha gavana wa Jiji la Nairobi lakini kufikia sasa hajapokea cheti cha uteuzi.

Hali hii sasa imemlazimu mbunge wa Makadara George Aladwa kujitosa kwenye mjadala huu na Kutaka chama hicho kitoe tikiti mara moja ili kumpa  Wanyonyi muda kuanza mikakati ya kushinda kiti cha ugavana katika uchaguzi wa Agosti.

“Ninaomba Bodi ya Kitaifa ya Uchaguzi ya ODM impe Tim Wanyonyi tikiti ya ugavana kama ilivyofanyika katika kaunti ya Kisumu, Migori, Homabay, Mombasa na Kakamega. Ndiye mgombeaji pekee na mwenye matumaini makubwa zaidi,” Aladwa alisema.

Aladwa alikuwa akizungumza siku ya Jumatatu, Aprili 18 alipoandamana na Wanyonyi kusambaza chakula cha msaada kwa familia 300 za Kiislamu kusherehekea Iftar.

Wanyonyi anatazamiwa kumenyana na Johnson Sakaja wa Kenya Kwanza ambaye tayari ametangazwa kuwa mgombeaji wa muungano wa Kenya Kwanza unaoongozwa na Naibu rais William Ruto.

Pia atachuana na mfanyabiashara Richard Ngatia (Jubilee) ambaye ameteua Philip Kaloki kama mgombe mwenza wake..

Chama tawala cha Jubilee kina wagombeaji, gavana wa sasa Anne Kananu, mfanyabiashara Agnes Kagure na Ngatia wanaotarajiwa kwenda kwa mchujo.

View Comments