In Summary

• Rais Uhuru Kenyatta ameshambuliwa Twitter kwa kuwataka walimu wakuu kumpigia makofi.

• Wakenya wampasha kwamba hakuna sababu ya kupigiwa makofi kwani maisha yamekuwa magumu katika uongozi wake.

rais Uhuru Kenyatta
Image: State House Kenya//Facebook

Rais Uhuru Kenyatta amezua gumzo kwenye mtandao wa Twitter baada ya kuwataka wananchi kumpigia makofi kutokana na kile alisema kwamba ametia juhudi kubwa kufanya kazi ya maana kwa ajili ya taifa hili.

Akizungumza katika kongamano la walimu wakuu wa shule za upili jijini Mombasa, rais Kenyatta aliwaambia walimu hao kwamba amewafanyia kazi kubwa ikiwemo kuwaongezea mishahara na kuajiri walimu wengine zaidi, na kwa hivyo kuwataka wampigie makofi ya rasharasha.

“Kwa kweli nimewasaidia sana nyinyi watu. Nimeajiri walimu, nimeongeza mishahara yenu, sasa mna bima. Pigeni kelele kwa viongozi wenu wajao lakini nipigieni makofi kwa kile nilichofanya. Tumeweka msingi wengine ili wengine wajao waendelee na ujenzi,” rais Kenyatta alisema.

Watumizi wa mtandao wa Twitter waliposikia matamshi hayo ya Kenyatta walifurika pale na kutumia maneno yake hayo kumkejeli.

“Makofi kwa mkuu ..Kenya ina bahati ya kuwa na wewe kama rais... tuna bahati sana tunalipa 75 bob kwa maziwa 500ml, bahati nzuri kwa akaunti zako za nje ya nchi, bahati ilibidi tupange mlolongo kutafuta mafuta, bahati nzuri sana. Kwa deni kubwa la umma, bahati sana kwa ufisadi, bahati nzuri kwa mauaji ya kiholela,” mmoja kwa jina la Kenneth Ndungu aliandika.

Wengine walitumia uhaba wa bidhaa kama vile Mafuta, maziwa na gharama ya juu ya mbolea pamoja na bidhaa zingine kumvua nguo hadharani, ila wana bahati rais hayupo kwenye mtandao huo kutokana na tangazo alilolisema miaka miwili iliyopita kwamab alifikia uamuzi wa kutoka Twitter kutokana na kukithiri kwa matusi dhidi yake.

View Comments