In Summary
  • Alitoa tangazo hilo Alhamisi katika makao makuu ya chama cha Jubilee jijini Nairobi
Sicily Kariuki ajiondoa katika kinyang'anyiro cha ugavana Nyandarua
Image: EZEKIEL AMINGA

Aliyekuwa Waziri wa Baraza la Mawaziri wa Maji Sicily Kariuki ametangaza kwamba amejiondoa katika kinyang'anyiro cha ugavana Nyandarua.

Alitoa tangazo hilo Alhamisi katika makao makuu ya chama cha Jubilee jijini Nairobi.

“Nilichukua uamuzi huu wa kijasiri baada ya kushauriana kwa mapana na kuwasikiliza wenyeji wa Nyandarua walioniomba nijitokeze kama mgombeaji wa uchaguzi ujao wa ugavana wa Nyandarua,” Kariuki alisema.

Kariuki aliandamana na mumewe Zabby Kariuki.

"Baada ya kutafakari, nilisimamisha nia yangu ya kuwania ugavana wa Nyandarua."

Hii sasa inamwacha Gavana aliye madarakani Francis Kimemia kuwa mgombeaji wa Jubilee Party.

Alikuwa akitafuta kumtimua Kimemia kwa tiketi ya chama cha Jubilee.

Waziri huyo wa zamani amewashukuru watu wa Nyandarua kwa kusimama naye tangu ajiunge na siasa, akisema kuwa watu mashinani wamekuwa wakisimama naye.

Alisema kuwa uamuzi wake ulikuja kufuatia makataa ya chama kukamilisha mchakato wa uteuzi na kuwasilisha majina kwa IEBC.

"Kuna wakati ambapo taifa ni muhimu zaidi kuliko mtu binafsi. Hapa ndipo nilipojipata kutoka wiki jana, kwamba tumekumbwa na mkwamo na makataa ya chama kuwasilisha orodha ya vyama kwa IEBC. "

 

 

 

View Comments