In Summary
  • DP Ruto kutangaza mgombea mwenza kabla ya Jumatatu wiki ijayo
  • Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Alliance ulichagua mahojiano ili kubaini mtu anayefaa kuwa naibu wa Raila
  • Mahojiano hayo yalianza Jumatatu, Mei 9 na yatakamilika Mei 10
DP RUTO
Image: DOUGLAS OKIDDY

Mwaniaji urais wa Muungano wa Kenya Kwanza na Naibu Rais William Ruto atatangaza mgombea mwenza wake kabla ya Jumatatu.

Akiongea na wanahabari katika makazi yake ya Karen siku ya Jumanne,Ruto alisema jina la mtu ambaye atakuwa naibu wake litawasilishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kabla ya tarehe ya mwisho iliyowekwa.

"Ninataka kuwahakikishia kuwa kama Kenya Kwanza na kama mgombeaji katika uchaguzi Mkuu ujao tutatuma mgombea mwenza wetu kwa IEBC kabla ya tarehe ya mwisho," Ruto alisema. .

IEBC inatarajiwa kupokea majina ya wagombea wenza waliopendekezwa na wawaniaji urais kufikia Mei 16.

Katika Muungano wa Kenya Kwanza unaoongozwa na Ruto, seneta wa Tharaka Nithi Kithure Kindiki, Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru, Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua na kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi ni baadhi ya viongozi wanaoaminika kuwania nafasi hiyo.

Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi, aliyejiunga na muungano wa Kenya Kwanza, pia ametajwa kuwa mgombea mwenza.

Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Alliance ulichagua mahojiano ili kubaini mtu anayefaa kuwa naibu wa Raila.

Mahojiano hayo yalianza Jumatatu, Mei 9 na yatakamilika Mei 10.

Gideon Moi wa Kanu alijiondoa kwenye mahojiano, huku chama chake kikimuidhinisha Kalonzo Musyoka.

Baada ya mahojiano, jopo la Azimio Running Mate Selection litatoa ripoti ya wagombea wanaofaa kwa baraza la Azimio na baada ya hapo mgombea atatangazwa.

 

 

 

View Comments