In Summary

• "Nimesema baada ya kufanya mihula miwili, nisingependa kuendelea tena. Ninahisi ni haki kuwaruhusu Wakenya wengine kuchukua unahodha wa chombo," alisema. 

the star

Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi ametangaza kuwa hana nia ya kuhudumu katika wadhifa huo katika Bunge litakaloundwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, 2022.

 "Nimesema baada ya kufanya mihula miwili, nisingependa kuendelea tena. Ninahisi ni haki kuwaruhusu Wakenya wengine kuchukua unahodha wa chombo," alisema. 

Muturi, akizungumza ya wanahabari bungeni, pia alifichua mipango ya kuongeza muda wa Bunge la tisa kwa angalau wiki moja. 

Alisema hii itakuwa kuwezesha kuanisha ratiba kabla ya kuahirishwa kwa vikao vya Bunge la Kitaifa na Seneti. 

"Haina maana kwamba Bunge ambalo linazingatia zaidi ya asilimia 95 ya sheria za kitaifa lirudi nyumbani mapema," Muturi alisema. 

Alikuwa na imani kuwa mengi yameimarika wakati wake kama spika na kuwataka wakenya na mashirika ya serikali kujitahidi kuelewa utendakazi wa Bunge.

 "Mahakama imekuwa ikitafsiri baadhi ya michakato yetu lakini tunapata kesi ambazo hazijathamini maana ya maamuzi," alisema. 

Bunge, kulingana na kalenda yake ya sasa, limesalia na vikao 12 tu huku kukiwa na msururu wa hoja muhimu ambazo lazima zisuluhishwe kabla ya mapumziko ya mwisho.

View Comments