In Summary

•Yohana Kisaka a ambaye anagombea kiti cha MCA  katika eneo bunge la Kanduyi alisema kuwa watu wanaoishi na ulemavu wametengwa kwa muda kwa shughuli vya kisiasa.

•Kisaka aliambia vyama vya kisiasa kujumuisha watu wanaoishi na ulemavu na kuwasaidia kutimiza ndoto zao ila sio kuwakandamiza.

Yonah Kisaka katika mkutano wa kisiasa uliofanyika katika soko ya Kanduyi mnamo Juni 13,2022
Image: TONY WAFULA

Watu wanaoishi na ulemavu (PLWD) kutoka Bungoma sasa wanataka wakaaji wa Bungoma kuwachagua katika viti mbalimbali vya kisiasa mwaka huu.

Yohana Kisaka anayeishi na ulemavu ambaye pia ni mgombea kiti cha MCA cha Township katika eneo bunge la Kanduyi alisema kuwa watu wanaoishi na ulemavu wametengwa kwa muda kwa shughuli vya kisiasa.

‘ Watu wanatuona kama kwamba hatuwezi kuingia katika ofisi za kisiasa na kushughulikia wananchi,nina uwezo wa kufanya kazi yoyote ya kiserikali’ Kisaka alisema.

Kisaka aliongeza kuwa aliingia katika siasa hili aweze kutetea haki ya watu

Alisema kuwa lazima watu wanaoishi na ulemavu  wahushishwe katika ugavi wa rasilimali.

‘Mkinichangua kuwa mwakilishi wadi katika bunge la kaunti ya Bungoma, nitahakikisha kuwa ajenda ya watu wanaoishi na ulemavu zimeshughulikiwa ipasavyo’alisema.

Kisaka aliambia vyama vya kisiasa kujumuisha watu wanaoishi na ulemavu na kuwasaidia kutimiza ndoto zao ila sio kuwakandamiza.

‘Kabla ya kukua mgombea huru, nilikuwa katika chama cha Jubilee, lakini wakati wa uteuzi wa chama, tiketi ilipewa mtu mwingine na mimi nikaachwa’ Kisaka alisema.

‘Niko na ndoto ya kuwa mwanasiasa tajika katika nchi hii,kuninyima tiketi haitauwa ndoto yangu, nitakuwa debeni  kama mgombea huru’

Kisaka ameapa kuwa atafanya kazi na gavana ambaye atachaguliwa kuhakikisha kuwa wakaazi wanapata manufaa ya serikali ya ugatuzi.

Alisema kuwa akichaguliwa atawasilisha hoja muhimu katika bunge la kaunti Bungoma zitakazowasaidia wakaazi.

Aliwarai wapiga kura kuchagua vijana wanaowania viti mbalimbali vya kisiasa.

‘Tukiwa shuleni walituambia kuwa sisi ndo viongozi wa kesho,sasa wakati umewadia na lazima tuwakilishe vijana katika siasa’

View Comments