In Summary
  • Mwanamuziki na mgombea mtarajiwa wa Ubunge wa Mathare Kevin Kioko Bahati amekanusha ripoti kwamba amejiuzulu kabla ya uchaguzi Mkuu wa Agosti
Image: INSTAGRAM// BAHATI

Mwanamuziki na mgombea mtarajiwa wa Ubunge wa Mathare Kevin Kioko Bahati amekanusha ripoti kwamba amejiuzulu kabla ya uchaguzi Mkuu wa Agosti.

Katika taarifa yake siku ya Jumatatu, Bahati alitaka kufafanua kuwa wanachama wachache wa Azimio La Umoja wamekuwa wakisababisha mkanganyiko miongoni mwa wafuasi wake kwa madai kwamba amejiuzulu - jambo ambalo si kweli.

“Mpendwa Azimio… acha kuwapotosha wapiga kura wa Mathare. Bahati - Mathare hajajiuzulu kwa ajili ya mtu yeyote. Puuza propaganda! #BAHATINEXTMPMATHARE 🙏,” Bahati Alitangaza.

Hii si mara ya kwanza kwa azma ya Bahati kuwawakilisha watu wa eneo bunge la Mathare kukumbwa na mkanganyiko na mabishano.

Mnamo Aprili, Bahati alitokwa na machozi baada ya Chama cha Jubilee kubatilisha cheti chake cha uteuzi kwa shinikizo la kutupilia mbali azma yake ya kumuunga mkono mgombeaji wa ODM na mbunge wa sasa Anthony Oluoch.

Akizungumza na vyombo vya habari, mkali huyo wa nyimbo za Mama alimwaga machozi alipotuma ujumbe kwa kiongozi wa chama cha Jubilee Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga, akiwataka wawape wakazi wa Mathare nafasi ya kumchagua mbunge wamtakaye.

 

 

 

View Comments