In Summary

•Mgombea  wa Urais Prof. Wajackoyah aliwaonya wanablogu kuacha  kutumia akaunti feki kwenye 'facebook ' kwa mnajili ya  kumchafulia jina lake.

•Akizungumza wakati wa uzinduzi wa manifesto yake, Mwanasiasa huyo aliweka wazi kuwa wanablogu  hao wataadhibiwa vikali atakapoingia ofisini mnamo tarehe 9 Agosti.

Profesa George Wajackoyah
Image: Youtube (Sceenshot)

Mgombea  wa Urais Prof. Wajackoyah aliwaonya wanablogu kuacha  kutumia akaunti feki kwenye 'facebook ' kwa mnajili ya  kumchafulia jina lake.

Alisema kuwa  wapinzani wake wanatumia hao mablogas kumharibia jina na kusema vitu visivyo vya ukweli  kumhusu kwenye  mtandao.

''Wengine wanajiita Prof. Wajackoyah kwa 'facebook' ile kizungu wanaandika haki ukisoma,eeh!! unajijazia'' Prof. Wajackoyah alisema.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa manifesto yake, Mwanasiasa huyo aliweka wazi kuwa wanablogu  hao wataadhibiwa vikali atakapoingia ofisini mnamo tarehe 9 Agosti.

Uzushi wa kublogi unahusishwa sana na mageuzi ya mtandao, ni dhahiri kwamba kublogi siku hizi kinachukuliwa kuwa taaluma na kukuwa na majukumu mbalimbali.

Kwanza, baadhi ya Wanasiasa na  Makampuni utumia sana  blogu  kama sehemu ya mkakati yao ya mawasiliano na pia kuuza bidha zao.

Wanablogu hutumia ukurasa yao kupeperusha habari mtandaoni,  kwa hivyo neno-ya-mdomo mtandaoni linaweza kuwa na nguvu sana kwani mtandao huwezesha kueneza habari mara moja duniani kote.

Uchapisho ya wanablogu mtandaoni yanaweza kuathirii mmoja au wengi kwa jumla haswa wakati  ambapo habari zinazochapishwa  si za ukweli.

Kwa hivyo, blogu kinaweza kuwa kifaa  chenye nguvu kulingana na habari iliyo nayo.

Mwanablogu ambaye akonauwezo wa  kuunda maudhui  ama habari za uongo kwenye mtandao, atakuwa katika nafasi bora  ya  kupata idadi kubwa ya wafuasi kushinda yule ambaye hafuati mtindo huo.

Wao pia  wanaruhusiwa kuandika kuhusu aina tofauti za maudhui,hii inachangia sana kwao kupata wafuasi wengi.

View Comments