In Summary

• Kositany, kwa utani alisema mwanafunzi aliyejibu kwamba toroli linaitwa UDA alijibu sawa.

Caleb Kositany Mbunge wa Soy
Image: Twitter

Mbung wa Soy Caleb Kositany aliibua utani katika mtandao wa Twitter baada ya kupakia picha moja ambaye imekuwa ikisambaa sana mitandaoni.

Picha hiyo ni ya karatasi la mtihani wa shule ya msingi inayoonyesha swali moja ambalo wanafunzi wametahiniwa kueleza majina ya vifaa vya shambani, mojawapo ikiwemo toroli.

Katika kile kiulifanya picha hiyo isambazwe pakubwa na kuzua vichekesho vingi, mwanafunzi ameandika majina ya vifaa vingine vizuri tu ila alipofika katika toroli, mwanafunzi aliipatia jina la UDA, ambacho ni chama cha naibu rais William Ruto chenye utambulisho wa nembo ya toroli.

Mbunge Kositany ambaye ni mwandani wa karibu sana wa William Ruto alifikiwa na picha hiyo ambayo inaonesha mwanafunzi alikosea kwa kuita toroli UDA na Kositany amemkosoa mwalimu vikali huku akisema kwamba mwanafunzi alikuwa anajua jibu sahihi kwani picha za nembo ya UDA zimesambaa pakubwa mpaka kwa watoto.

“Hii inafaa kurudiwa katika kusahihishwa. Mwanafunzi amejibu vizuri,” Kositany aliandika kwa utani huku akimalizia na emoji za kucheka na kuvunja mbavu.

Picha hiyo ikiambatanishwa na maneno ya Kositany iliwavunja mbavu wengi huku wengine wakisema huyo mwanafunzi ni mfuasi wad amu wa naibu rais William Ruto huku wengine waliokosa kuelewa utani katika picha hiyo wakizua kebehi za kisiasa kutupiana mabomu ya maneno moto.

Chama cha UDA kwa muda mrefu kimejipata katika hali ngumu huku wapinzani wa kisiasa wa naibu rais wakisema kwamba kiongozi huyo anapanga kuchukuwa urais ili kuanza kuwapatia watu matoroli ili kufanyia kazi.

Si mara moja au mbili naibu rais amejitokeza kujitetea dhidi ya madai hayo huku akisema kwamba toroli limetumika tu kama nembo ya utambulisho wa chama na wala si kifaa cha shambani anachopanga kuwapa wafuasi wake, akitolea mfano wa vyama vingine kama kile chenye nembo ya simba na kusaili kama kweli nacho kinapanga kuwapatia wafuasi wake simba.

View Comments