In Summary
  • Viongozi hao walidai kuwa katika manifesto yake, mkuu wa pili hakuonyesha jinsi alivyokusudia kupambana na ufisadi
DP RUTO
Image: EZEKIEL AMING'A

Naibu Rais William Ruto amewasuta  viongozi wa muungano wa Azimio la Umoja kuhusu msimamo wao wa kupigana na ufisadi.

Akizungumza huko Sololo, kaunti ya Marsabit, Jumatano, Ruto alisema kiongozi wa Azimio Raila Odinga amekuwa akila na wafisadi na hata anatumia mapato ya ufisadi kufanya kampeni.

"Acheni uhuni, hamna kazi ya kutupa msomo kuhusu ufisadi na huku mnatumia fedha za wafisadi kufanya kampeni, huwezi kuwa unakula na wafisadi na kutoa hutuba dhidi ya rushwa,” alisema.

DP alidai kuwa Raila amekuwa akiwakinga magavana ambao wana kesi za ufisadi.

"Wacha kuongea mambo ya ufisadi, wewe ndio umewakinga magavana ambao wameiba pesa za umma. Wanakuja kwako unawaficha ili mgawane ile pesa wameiba."

Aliongeza;

"Leo Wakenya wanalalamika, IMF inalalamika, mkaguzi mkuu wa mahesabu analalamika, pesa za Covid, Shilingi bilioni 10 na bilioni 65 kutoka IMF zilipotea chini ya uangalizi wa serikali ya handshake."

Matamshi ya naibu rais yamechochwa na mashambulizi ya viongozi wa Azimio kuwa Ruto hana mpango au nia ya kukabiliana na ufisadi.

Viongozi hao walidai kuwa katika manifesto yake, naibu rais hakuonyesha jinsi alivyokusudia kupambana na ufisadi.

 

 

 

 

 

View Comments