In Summary
  • Ruto alisema ni mapenzi ya Mungu kwamba kanisa linasaidia kuwaunganisha Wakenya wakati huu, kupitia usaidizi wao
  • Aliapa kuhakikisha kuwa siasa za migawanyiko hazitakuwa na nafasi katika taifa iwapo atachaguliwa Agosti 9
DP RUTO
Image: EZEKIEL AMING'A

Mgombea urais wa UDA William Ruto Ijumaa alikariri matamshi kwamba uongozi wake utalilinda kanisa iwapo atajinyakulia kiti cha urais mwezi Agosti.

Akizungumza kwenye hafla ya ushirika na makasisi wa kaunti ya Nakuru huko Ngata, Ruto aliwaahidi viongozi wa kanisa hilo kuwa hatawaangusha, akiwashukuru kwa kuendelea kumuunga mkono.

"Asante sana kwa kutuombea. Hujui umetufanyia nini, kwa maombi haya rahisi tu."

"Tutasimama juu ya imani na tutahakikisha Kenya inaendelea kuwa ni nchi ambayo inamcha Mungu... Tutalilinda na kulitetea neno la Mungu nchini Kenya," alisema.

Ruto alikiri kuwa safari ya kuwaunganisha Wakenya, kati yake na bosi wake Rais Uhuru Kenyatta ilianza Nakuru.

DP alipongeza kwamba viongozi wa kidini kwa kuchagua upande, na kuongeza kuwa Biblia ilipendekeza hilo.

“Nataka niwapongeze kanisa, hamjakwepa kuegemea upande mmoja, mnajua neno la Mungu linasema mtu asiwe vuguvugu ni bora awe moto au baridi,” alisema.

Ruto alisema ni mapenzi ya Mungu kwamba kanisa linasaidia kuwaunganisha Wakenya wakati huu, kupitia usaidizi wao.

Aliapa kuhakikisha kuwa siasa za migawanyiko hazitakuwa na nafasi katika taifa iwapo atachaguliwa Agosti 9.

 

 

 

 

View Comments