logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sakaja kuwania ugavana wa Nairobi huku jina la Sonko likikosekana kwenye orodha ya IEBC

Tume ya IEBC pia ilikuwa imemzuia Sonko kuwania ugavana kufuatia kutimuliwa kwake 2018.

image
na Radio Jambo

Makala10 July 2022 - 12:27

Muhtasari


  • Haya yanajiri licha ya uamuzi wa mahakama kuu kuja Jumanne ambao utaamua kujumuishwa kwa jina la Nairobi Sakaja kwenye karatasi za kupigia kura
Mgombea Ugavana wa Naairobi Johnson Sakaja mbele ya Kamati ya IEBC ya Kusuluhisha Mizozo katika Mahakama ya Milimani mnamo Juni 15 2022.

Mgombea Ugavana wa Nairobi Johnson Sakaja ametangazwa rasmi kuwa mgombea Ugavana na IEBC.

Haya yanajiri licha ya uamuzi wa mahakama kuu kuja Jumanne ambao utaamua kujumuishwa kwa jina la Nairobi Sakaja kwenye karatasi za kupigia kura.

Katika notisi ya gazeti la serikali, Sakaja amechapishwa pamoja na mgombea mwenza wake Njoroge Muchiri kama wagombeaji wa chama cha United Democratic Alliance (UDA).

Sakaja sasa ni miongoni mwa majina 16,100 ambayo yalikuwa yametumwa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Wafula Chebukati kwa ajili ya kutangazwa kwenye gazeti la serikali mnamo Juni 30, 2022.

Mgombea kiti cha Ugavana wa Mombasa Mike Sonko jina lake halijajumuishwa katika orodha ya wagombeaji watakaoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Agosti.

Haya ni kulingana na notisi ya gazeti la serikali ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Jumapili, ikionyesha majina ya wagombeaji wote wa Urais, Ugavana, Useneta na Wabunge ambao watapigIwa kura kwenye uchaguzi wa Agosti 9.

Jina la Sonko haliko katika orodha hiyo kutokana na ukweli kwamba ana kesi inayosubiri kuwasilishwa mbele ya benchi ya majaji watatu katika mahakama moja mjini Mombasa, na mahakama ya mizozo ya IEBC bado haijamuidhinisha kugombea.

Kulingana na mahakama hiyo, Sonko alikosa kuwasilisha cheti chake halisi cha digrii pamoja na nakala yake iliyoidhinishwa, kinyume na kifungu cha 75 cha katiba ya Kenya.

Mahakama hiyo pia ilisikia kwamba ingawa Sonko alikuwa amewasilisha nakala ambazo zilikuwa zimeidhinishwa na wakili wake wakati wa uchaguzi uliopita  hitaji la digrii katika 2022 lilitumika kwa wagombeaji wote.

Tume ya IEBC pia ilikuwa imemzuia Sonko kuwania ugavana kufuatia kutimuliwa kwake 2018.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved