In Summary

• Mwanasiasa huyo alisema IEBC ikikaidi kumjumuisha kwenye kinyang'anyiro chqa urais basi wajiandae kwa marudio ya uchaguzi.

Mgombea urais Ruben Kigame
Image: Facebook//Ruben Kigame

Mahakama ya juu kwa mara nyingine imefanya uamuzi wa kusua gumzo nchini Kenya baada ya kuitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kumruhusu mgombea urais Ruben Kigame kugombea urais.

Katika uamuzi huo uliotolewa Jumatatu, Kigame alikuwa ameelekea mahakamani kutaka uamuzi wa IEBC kumfungia nje ya kinyang’anyiro cha urais kufutiliwa mbali na kuruhusiwa kuwania katika kivumbi hicho cha Agosti 9.

Jaji Anthony Mrima alisema Kigame sasa yuko huru kupeleka vyeti vyake mbele ya tume ya IEBC ili kutathminiwa kabla ya kuruhusiwa kujiunga na wenzake watatu David Mwaure, George Wajackoyah, Raila Odinga na William Ruto katika kipute hicho cha urais siku ishirini zijazo.

Ruben Kigame ambaye ni maarufu kutokana kwa nyimbo zake za kutukuza Mungu alipokea uamuzi huu kwa furaah na kusema kwamba ushindi huo ni ushindi kwa kila mtu.

“Ni ushindi hata kwa wale ambao hawana Imani. Ni ushindi kwa Wakenya ambao wamechoka haswa na wale wagombea ambao walikuwa wamepewa, kwa sababu tulikuwa tumefinyiliwa na kuchagua kati ya wagombea wanne tu na hasa wale wawili wa juu ambao wamepigiwa debe sana, kwa hiyo huu ni ushindi kwa wale ambao walisema hawatapiga kura kama mimi siko debeni,” alisema Ruben Kigame.

Kigame aliishukuru mahakama ya juu kwa kupitisha uamuzi wa maana na kusema kwamba ikiwa jinsi ambavyo IEBC ilikuwa inasema kwamba tayari wameshachapisha karatasi za kupiga kura basi litakuwa jambo la kusikitisha mno kwani jaji mkuu Martha Koome hatua hiyo haikufaa kuchukuliwa hadi kesi zote ziamuliwe.

Mgombea huyo aliitaka tume ya IEBC kufuata sheria na kuepusha marudio ya uchaguzi kwa sababu kulingana na yeye, tume hiyo isipomuweka kwenye karatasi za kupiga kura basi uchaguzi utarudiwa.

“Ni rahisi kuniongeza kwenye karatasi za kupiga kura kuliko kurudia uchaguzi mzima. Itakuwa rahisi kuchapisha ile karatasi moja yenye mimi nimeongezwa kuliko kulazimika kuchapisha karatasi zote,” alisema Kigame.

Alimtaka mwenyekiti wa IEBC na makamishna wake kuhakikisha wametii uamuzi wa mahakama na kama la hawajatii basi atajua fika kwamba wanamchukia na pia wana chuki kubwa kwa watu wanaoishi na ulemavu ambao katiba ya mwaka 2010 inatetea.

Sasa inasubiriwa kuonwa kama IEBC itatii uamuzi wa mahakama au la.

View Comments