Mgombea urais wa Kenya Kwanza William Samoei Ruto amesema kuwa rais Uhuru Kenyatta huenda anamtakia mema katika kinyanganyiro ya urais.
Akizungumza mjini Eldoret siku ya Jumatatu tarehe moja Agosti, Ruto alirejelea hotuba ya rais jana wakati wa uzinduzi wa barabara ya mwendokasi kama maneno yanayo mpa nguvu na matumaini ya kufikisha ndoto yake ya kukuwa rais wa tano wa Kenya.
Ruto hakusita kujipigia debe na kusema kuwa yeye ndiye atakaye shika ushukani baada ya kushinda mpizani wake wa karibu Raila Amollo katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
''Nyote mlimsikia jana (jumapili), sivyo? Hapo awali, alisema kuwa hatawahi kukabidhii mamlaka kwa William Ruto, lakini jana akasema kuwa atakabidhii mamlaka kwa yeyote atakayeshinda uchaguzi,'' Ruto alisema.
Alichukua nafasi hiyo pia kupongeza rais Uhuru Kenyatta kukuwa katika mstari wa mbele kupigania demokrasia ya nchi,baadaye akadokeza kuwa atamtuma nyumbani pamoja na mgombea wa urais wa Azimio one Kenya Raila Odinga.
''Pia nilikusikia ukisema kwamba yeyote atakayepoteza, ataenda na wewe nyumbani . Sasa jiandae na uweke mzigo wako Kitendawili kwenye 'Wheelbarrow' na umpeleke nyumbani'' Ruto alisema.
Naibu rais alikuwa akimjibu rais baada ya kujitenga na uvumi kwamba alikuwa akipanga kumuua naibu wake na wanasiasa wote wanaomuunga mkono.
Kiongozi huyo wa Kenya kwanza pia alikashifu kufungwa kwa uwanja wa Bukhungu na kusema kuwa hiyo ni ishara tosha ya kutokomaa kisiasa kwa upande wa wapinzani wao.
''Wewe Raila nataka ni kwambie kwamba tukienda Nyanza, watu wako watakuballiana na sera zetu, nataka niwahakikishie wananchi wa mkoa huo kuwa hatutawaacha nje ya serikali , inasikitisha kwamba hatuwezi kuenda Nyanza sai, lakini wakaazi wa hapa Eldoret walikukaribisha vizuri, kumanisha sisi si watu wa vita'' Ruto alisema.