In Summary

•Infotrak ilieleza kuwa ikiwa Raila angeweza kupata nusu ya kura ambazo hazijaamuliwa, angeshinda uchaguzi katika awamu ya kwanza na asilimia 52, sawa na kura milioni 11.4.

Kinara wa ODM Raila Odinga na Kinara wa UDA William Ruto
Image: Maktaba

Kura ya maoni ya mwisho iliyotolewa na Infotrak Jumatano jioni, Agosti 3, inaonyesha kinara wa urais wa Azimio La Umoja, Raila Odinga, angeshinda katika takriban kaunti 24 ikiwa uchaguzi ungefanyika leo.

Utafiti huo ulionyesha kuwa ikiwa idadi ya wapiga kura itafikia asilimia 99, Raila angeshinda kura nyingi kati ya milioni 10.8 katika kaunti 24.

Infotrak ilieleza kuwa ikiwa Raila angeweza kupata nusu ya kura ambazo hazijaamuliwa, angeshinda uchaguzi katika awamu ya kwanza na asilimia 52, sawa na kura milioni 11.4.

Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kinachoongozwa na Naibu Rais William Ruto na Rigathi Gachagua kinaongoza katika kaunti 17 zilizo na wapiga kura milioni 9.3 waliosajiliwa.

Kura hiyo ya maoni  ilionyesha kuwa ikiwa idadi ya wapiga kura itafikia asilimia 99, Ruto atapata kura nyingi kati ya milioni 9.3 za kaunti hizo.

Utafiti hiyo  iliendelea kuonyesha kwamba hata kama Ruto angeshinda asilimia 100 ya kura ambazo hazijaamuliwa, bado hangenyakua urais kwa vile hangepata asilimia 50 pamoja na kura moja.

Matokeo hayo pia ilidhihirisha kuwa , Ruto angepata asilimia 45 ya kura zote.

Matokeo ya kura ya maoni yalitolewa kutoka kwa waliojibu ambao walithibitisha kuwa watashiriki uchaguzi wa Agosti 9.

Kura hiyo ya maoni pia ilionyesha kuwa umaarufu wa Raila uliongezeka kutoka asilimia 49 hadi 53 na huku wa Ruto ukiongezeka kutoka asilimia 41 hadi 45 katika kura ya awali iliyojumuisha wapiga kura ambao hawajaamua.

 

View Comments