logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jina la Ngilu laonekana kwenye karatasi za kupiga kura licha ya kujitoa awali

Takriban miezi miwili iliyopita, wakati wa kampeni za muungano pana wa Azimio la Umoja One Kenya, kinara wao Raila Odinga alitangaza kwamba angempa Ngilu kazi katika serikali kuu

image
na Davis Ojiambo

Uchaguzi09 August 2022 - 12:31

Muhtasari


  • • Katika baadhi ya picha za karatasi za kupiga kura hizo ambazo zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, jina la Ngilu linaonekana kwenye karatasi za ugavana
PAMOJA gavana wa Kitui Charity Ngilu na mwaniaji ugavana David Musila katika hafla ya awali katika mji wa Kitui.

Sintofahamu ilikumba macho ya wapiga kura kaunti ya Kitui baada ya jina la gavana wa sasa Charity Ngilu kuonekana kwenye karatasi za kupiga kura licha ya gavana huyo kuweka wazi wiki kadhaa zilizopita kwamba amejitoa katika kinyang’anyiro hicho.

Katika baadhi ya picha za karatasi za kupiga kura hizo ambazo zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, jina la Ngilu linaonekana kwenye karatasi za ugavana za kupiga kura likiwa la mwisho pamoja na mgombea mwenza wake Gideon Nzau, huku waliokuwa wakimenyana naye kwenye kipute cha ugavana Kitui wakiwa ni gavana wa kwanza Julius Malombe ambaye aliwania na Wiper, Jonathan Mueke wa UDA na David Musila wa Jubilee.

Takriban mwezi mmoja uliopita, wakati wa kampeni za muungano pana wa Azimio la Umoja One Kenya, kinara wao Raila Odinga alitangaza kwamba angempa Ngilu kazi katika serikali kuu na kutangaza kwamba Kitui wangemuunga mkono gavana wa zamani Julius Malombe.

Inaarifiwa baadae Ngilu aliwataarifu wakaaji wa Kitui kutompigia kura kwani sasa ashaweka pembeni azma yake ya ya kuwania kipindi cha pili kama gavana na badala yake kuwataka wampigie kura malombe.

Inaarifiwa IEBC ilisema kwamba kipindi cha kutangaza kujitoa kwake katika kinyang’anyiro cha ugavana, tayari karatasi za kupiga kura zilikuwa zimepigwa chapa na majina ya wagombea wote ugavana wakiwa wamewekwa pamoja na nembo za vyama vyao.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved