In Summary

• Ojaamong alimtakia mafanikio Otuoma akisema anafaa kuwa tayari kuwatumikia waliompigia kura na wale ambao hawakumpigia kura.

Gavana wa Busia anaeondoka Jospeter Odeke Ojamoo

Gavana wa Busia anayeondoka Sospeter Ojaamong amekubali kushindwa katika kinyang'anyiro cha ubunge wa Teso Kusini.

Ojaamong, ambaye muhula wake wa pili kama Gavana pia umekamilika, alitumia mitandao ya kijamii kuwapongeza washindi katika uchaguzi wa Agosti 9.

“Uchaguzi umekwisha, lakini kanuni zetu zitadumu kwa vizazi. Kwa familia yangu, marafiki, timu, na kampeni, Asante kwa usaidizi usioyumbayumba wakati wa utawala wangu na kipindi cha kampeni. Nimetiwa moyo na kunyenyekea kwa usaidizi wenu,” aliandika.

Ojaamong vile vile alimpongeza Paul Otuoma, ambaye anakaribia kushinda kinyang'anyiro cha Ugavana wa Busia.

"Umeanza sura mpya maishani mwako. Harakati za upokezaji wa mamlaka zitafanywa kwa kwa njia shwari, ili uanze kazi. Kwa wakati ufaao nitakualika kwa afisi ya gavana kwa madhumuni ya kufahamiana na kutwaa madaraka chini ya Katiba yetu na sheria ya serikali ya kaunti,” Ojaamong aliambia Otuoma.

Ojaamong alimtakia mafanikio Otuoma akisema anafaa kuwa tayari kuwatumikia waliompigia kura na wale ambao hawakumpigia kura.

“Ni wachache sana watakao kuwa na heshima ya kujua wajibu unaohisi sasa. Ni wachache sana wanaojua msisimko wa wakati huu na changamoto utakazokabiliana nazo,” Gavana huyo anayeondoka alisema.

Gavana huyo wa Busia anayeondoka pia alionya Otuoma kuwa kutakuwa na nyakati za majaribu na kwamba watu anaowachukulia kuwa marafiki watamvunja moyo.

“Lakini, utakuwa na Mungu Mwenyezi wa kukufariji, familia inayokupenda, na Kaunti ambayo itakuwa ikivuta kwa ajili yako, nikiwemo mimi. Haijalishi kitakachotokea, utatiwa moyo na tabia na huruma ya watu utakaowaongoza,” aliambia Otuoma.

View Comments