In Summary

•Lupita pia amewashukuru wakazi wa Kisumu hata kabla ya matokeo rasmi ya ugavana kutangazwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC).

•Nyong'o alidokeza ushindi wake na kueleza imani yake kuwa muungano wa Azimio la Umoja utatwaa uongozi wa Kenya.

Lupita Nyong'o na babake Anyang' Nyong'o
Image: HISANI

Muigizaji maarufu Lupita Nyong'o amempongeza baba yake Peter Anyang Nyong'o kwa kushinda kiti cha ugavana Kisumu kwa muhula wa pili.

Lupita pia amewashukuru wakazi wa Kisumu hata kabla ya matokeo rasmi ya ugavana kutangazwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC).

"ABICH MORO! Hongera kwa baba yangu na ASANTE kwa watu wa Kisumu kwa uungwaji mkono mkubwa kwenye kurai @AnyangNyongo," Lupita alisema kupitia ukurasa wake waTwitter.

Muigizaji huyo alichukua hatua ya kumpongeza babake Jumatano jioni huku matangazo rasmi ya matokeo ya ugavana Kisumu yakiendelea kusubiriwa.

Hapo awali, Nyong'o alidokeza ushindi wake na kueleza imani yake kuwa muungano wa Azimio la Umoja utatwaa uongozi wa Kenya.

"Mungu amefanya tena, atafanya pia kwa Azimio. Ushindi wa asilimia 80. Mungu Mbele!" Nyong'o alisema kupitia Twitter.

Gavana huyo alikuwa akikuwa anatetea kiti chake kwa tiketi ya chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga.

Alikuwa akimenyana na Jack Ranguma wa Movement for Democracy and Growth (MDG), Bi Awuor Meso na Tom Ndalo.

View Comments