logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Huu ndio ushindi Marehemu mke wangu anakosekana, Mungu amlaze pema - Boni Khalwale

“Naweka wakfu ushindi huu wangu kwa marehemu mke wangu mpendwa Mungu amlaze mahala pema palipo wema, alikuwa amesimama na mimi katika miaka 20 ya kushinda, ni katika ushindi huu tu ambapo amekosekana,” Daktari Boni Khalwale

image
na Davis Ojiambo

Uchaguzi13 August 2022 - 12:50

Muhtasari


  • “Naweka wakfu ushindi huu wangu kwa marehemu mke wangu mpendwa Adelaide Shikanga Khalwale," - Khalwale.
Boni Khalwale, seneta mteule wa Kakamega

Seneta mteule wa Kakamega Boni Khawale katika hafla ya kukabidhiwa cheti baada ya kutangazwa kushinda uchaguzi kwenye kaunti hiyo kupitia tikiti ya chama cha UDA aliacha wengi katika machozi ya furaha.

Khalwale aliwashukur watu wote katika kaunti hiyo pana mkoa wa Magharibi kwa kumpigia kura bila kuangalia chama kwani eneo hilo liliwapigia watu wengi kura kutoka muungao wa Azimio la Umoja One Kenya ilhali yeye aliwania kutoka Kenya Kwanza na kuchaguliwa.

“Nataka kuwashukur watu wa Kakamega kwa sababu mlipiga kura kando na vyama vya kisiasa, mlipiga kura kando na ukabila katika kaunti hii na pia mmeipa Kenya nafasi kuonesha kwamba kila kitu kinawezekana,” Khalwale alisema huku akiongeza kwamba amenyenyekea sana kuteuliwa.

Akionekana kulemewa na hisia, Khalwale alikumbuka jinsi alivyosimama katika ukumbi huo miaka kadhaa iliyopoita alipoibuka kama mwanafunzi bora na kuitwa chuo kikuu cha Nairobi kusomea udaktari, ndoto ambayo baada ya kufuzu aliiacha na kuingia kweney siasa akiwa na Imani kwamba hata mtoto wa maskini naye anaweza pata nafasi katika uongozi.

“Nilichukua njia hii ili kwa watu wa Kakamega kuacha kitivo change nikiamini kwamba hata mtoto wa maskini ana nafasi katika nchi hii, mama yangu alikuwa muuza pombe, na babangu alikuwa muuza miwa katika soko la Marinya, na ndio maana nimefika hapa, walikuwa ni wazazi wenye kujivunia sana,” Khalwale alizungumza.

Mwanasiasa huyo pia alimsifia mkewe marehemu na kusema kwamba ushindi huo ni kwa ajili yake. Khalwale alisema kwamba marehemu mkewe alisimama na yeye katika miaka zaidi ya 20 akiongozi na safari hii ndio mara ya kwanza anashinda pasi na kuwepo kwa mkewe.

“Naweka wakfu ushindi huu wangu kwa marehemu mke wangu mpendwa Adelaide Shikanga Khalwale, Mungu amlaze mahala pema palipo wema, alikuwa amesimama na mimi katika miaka 20 ya kushinda, ni katika ushindi huu tu ambapo amekosekana,” Daktari Boni Khalwale alizungumza kwa hisia.

Hii si mara ya kwanza Khalwale anamsifia wazi mkewe marehemu na itakumbukwa mwezi mmoja uliopita wakati mjukuu wake alipozaliwa, alisherehekea kwa kusema kwamba mtoto huyo ni kama kurudi upya au kuzaliwa kwa marehemu mkewe Shikanga.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved