logo

NOW ON AIR

Listen in Live

IEBC yafuta kura 10K za Kiambu zilizohesabiwa kimakosa kwa upande wa DP Ruto

Hapo awali, Tume ilitangaza kuwa DP Ruto wa UDA alikuwa akiongoza katika eneo bunge hilo kwa kura 51,050 dhidi ya 14,860 za Raila licha ya kura zote halali kuwa 56,546.

image
na Davis Ojiambo

Uchaguzi13 August 2022 - 09:55

Muhtasari


  • •"Katika Msingi wa Thindigwa ilinaswa kwamba 11 walimpigia kura Odinga badala ya 111. Hilo limesahihishwa katika Fomu C."
  • •Hapo awali, Tume ilitangaza kuwa DP Ruto wa UDA alikuwa akiongoza katika eneo bunge hilo kwa kura 51,050 dhidi ya 14,860 za Raila licha ya kura zote halali kuwa 56,546.
Kamishna wa IEBC Justus Nyang'aya akiwa Bomas of Kenya mnamo Agosti 12,2022.

IEBC Jumamosi iliripoti kura 10,000 zilizotiliwa shaka ambazo zilihesabiwa kimakosa kumuunga mkono Naibu Rais William Ruto kutoka Eneo Bunge la Kiambu Mjini.

Awali, Tume ilitangaza kuwa Naibu Rais Ruto wa UDA alikuwa akiongoza katika eneo bunge hilo kwa kura 51,050 dhidi ya 14,860 za Raila licha ya kura zote halali kuwa 56,546.

David Mwaure na George Wajackoyah walipata kura 318 kila mmoja.

Idadi ya awali iliyotangazwa na Kamishna Justus Nyangaya siku ya Jumamosi ilikuwa kura 10,000 zaidi ya kura zilizopigwa.

Hata hivyo hilo lilirekebishwa baada ya waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo kwa Tume.

Akifanya masahihisho hayo, Nyang'aya alisema Ruto alipata kura 41,050 badala ya kura 51,050 kama ilivyotangazwa awali.

"Katika fomu 34B kulikuwa na makosa, ambayo yalisahihishwa katika fomu 34C, Katika Msingi wa Thindigwa ilinaswa kuwa 11 walimpigia kura Odinga badala ya 111. Hilo limesahihishwa katika Fomu C," alifafanua.

Tafsiri: MOSES SAGWE


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved