Linet chepkorir ‘Toto’, anakuwa Mwanamke mwenye umri mdogo zaidi kuwa mwakilishi Bungeni.
Hii ni kazi yake ya kwanza kabisa, Anatoka katika familia yenye uwezo wa hali chini, akiwa ni mtoto wa tatu kwa Bwana Richard langat na mkewe Bety langat.
Linet anatarajia kuboresha makazi yake na kufanya maisha ya wazazi wake kuwa bora zaidi. Hakuna huduma ya umeme katika kijiji chakewa Bwana Richard langat na mkewe Bety langat.
Linet anasema ilikuwa ngumu kupambana dhidi ya washindani wenye mifuko mirefu, anakadiria kutumia kiasi cha shilingi ya kenya100,000 pekee kufanya kampeni na nyingine zilitoka kwa watu waliomtakia mema na marafiki wenye nia nzuri katika kisiasa.
Ilikuwa ni shamrashamra, furaha, ngoma na machozi wakati kijiji kikimkaribisha nyumbani kwake, changamoto kubwa alipoanza mchakato wa kugombea ilikuwa ni kuishawishi jamii yake na wapiga kura kwa ujumla ambao walihoji kuwa hawezi kufanya hivyo kwa sababu hajaolewa, hana uzoefu wa kazi na hana pesa za kutoa.
Ujumbe wake kwa wasichana wote ‘usikate tamaa kamwe