Mgombea urais wa muungano wa Azimio One Kenya Raila Odinga anaongoza katika eneo bunge la Embakasi Mashariki, kaunti ya Nairobi, mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema.
Raila alipata kura 53,982 huku mgombea urais wa UDA William Ruto akipata kura 30,976.
David Waihiga wa Chama cha Agano alipata kura 271 huku mshika bendera wa Roots Party George Wajackoyah akiwa na kura 388.
Mwenyekiti wa IEBC alisema kulikuwa na wapiga kura 154,599 waliosajiliwa katika eneo bunge hilo.
Jumla ya kura halali zilizopigwa ni 85,623 huku kura 492 zilikataliwa.
IEBC pia itathibitisha kura za diaspora kabla ya kutoa hesabu ya mwisho.