Seneta wa Bungoma Moses Wetang'ula amechaguliwa tena.
Matokeo yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka yalionyesha kuwa bosi wa Ford Kenya alipata kura 286,143.
Chama cha Ford-Kenya kinachoongozwa na Wetangula ni mshirika katika muungano wa Kenya Kwanza unaoongozwa na Naibu Rais William Ruto.
Naibu gavana wa Bungoma anayeondoka Charles Ngome, mwanahabari Advice Mundalo na mwanasiasa Machacha Machembe walikuwa wametupa kofia zao ulingoni kwa nia ya kumtimua Wetangula.
Machacha hadi sasa amekubali kushindwa na kuwashukuru, hasa watu wa Sirisia, ambao alisema walisimama naye.
"Nataka kuwashukuru wote waliosimama nami na kunipigia kura, hasa Sirisia, ambako nilipata kura 21,000," Machacha alisema.
Mnamo Agosti 10, Machacha alimsifu Wetangula kwa ushindi mkubwa wa kuhifadhi kiti chake.
"Kulingana na matokeo ya awali yanayotiririka, inaonyesha kuwa Wetang'ula anachukua kiti hiki mapema sana," alisema.
"Uchaguzi sio wa kupigana, wacha washiriki wengine katika nyadhifa zingine wakubali matokeo ya kura na waunge mkono wale walioshinda."