In Summary

•Kama kawaida yake ya kuwa katika ofisi tofauti ya kisiasa, Sakaja aliamua kuwania kiti cha ugavana katika uchaguzi uliopita  wa Agosti 9,na kushinda mpizani wake wa karibu Paul Igathe.

Mwanasiasa Sakaja
Image: Star

Gavana mteule wa Nairobi Johnson Sakaja amewekawazi kuwa ndoto yake ya kuingia katika sasa ilichochewa na azma yake ya kuwa rais wa nchi hii.

Sakaja ambaye alikuwa Seneta wa zamani ya kaunti ya Nairobi alichaguliwa kama gavana wa sasa wa Nairobi ambapo anatarajiwa kuapishwa rasmi na mgombea mwenza wake hapo kesho.

''Nikiwa mtoto mdogo nilikuwa na ndoto ya kuwa rais, lakini kwa sasa niko na kazi ya kuhudumia wakaaji wa Nairobi, labda nikimaliza kazi yangu ya ugavana, wao ndo watanieleza ni wapi nitaelekea, lakini kwa sasa sitilii manane sana kuhusu  ndoto hilo ya kuwa rais'' Sakaja alisema.

Mwanasiasa huyo amepiga hatua mingi katika nyanja ya kisiasa na kupanda mataraja tofauti tofauti kwa lengo ya kujenga tarjiba yake kama mwanasiasa.

Mnamo 2007, alichangia sana kurai vijana  kumuunga mkono rais wa zamani Mwai Kibaki .

Hii ilifungua njia yake kwa siasa za kitaifa tangu alipojiunga na timu ya Kibaki kwa uchaguzi wa 2007  kama mmoja wa mrengo huo.

Baadaye akawa mkurugenzi wa kikundi cha Vijana na Kibaki, kitu kilicho mfanya kuchaguliwa kuwa mmoja wa maajenti katika kujumlisha kura  za urais kwa uungaji mkono mkubwa wakati wa uchaguzi hiyo.

Baada ya serikali ya Kibaki, mwanasiasa huyo alijitosa katika kinyanganyiro cha Useneta na kushinda katika uchaguzi hiyo na kuwa Seneta wa Nairobi.

Kama kawaida yake ya kuwa katika ofisi tofauti ya kisiasa, Sakaja aliamua kuwania kiti cha ugavana katika uchaguzi uliopita  wa Agosti 9,na kushinda mpizani wake wa karibu Paul Igathe.

 

View Comments