logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto na Rachel waelekea Bomas ambako matokeo ya urais yanatarajiwa kutangazwa

Chebukati katika taarifa yake alisema tume itamtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais Jumatatu saa tisa alasiri.

image
na Radio Jambo

Makala15 August 2022 - 10:26

Muhtasari


•Chebukati katika taarifa yake alisema tume ya uchaguzi na mipaka itamtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais Jumatatu saa tisa alasiri.

Naibu Rais William Ruto awasili Bomas ya Kenya

Naibu Rais William Ruto na mkewe Rachael Ruto wameondoka nyumbani kwao Karen kuelekea Bomas of Kenya kabla ya matokeo ya urais kutangazwa na IEBC.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati katika barua kwa vyombo vya habari alisema tume ya uchaguzi na mipaka itamtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais Jumatatu saa tisa alasiri.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inakualika kuangazia tangazo la Matokeo ya Urais mnamo Jumatatu Agosti 15, 2022 katika Bomas of Kenta saa tisa alasiri," Barua iliyoachiwa na IEBC ilisoma.

Chebukati anatarajiwa kumtangaza rais mpya wa Kenya baada ya shughuli ya uhakiki wa fomu za matokeo ya urais kutoka maeneobunge yote na ujumuishaji wa kura  kukamilika.

Uhakiki wa fomu za matokeo ya uchaguzi wa Agosti 9  ulikamilika Jumatatu asubuhi baada ya kuendelezwa kwa siku tano.

Hapo awali, kiongozi wa Roots Party George Wajackoyah na David Mwaure wa Agano walifika katika ukumbi wa Bomas of Kenya kabla ya kutangazwa rasmi kwa matokeo.

Kwa sasa, kwaya ya kikatoliki inawaburudisha wanasiasa na waalikwa wengine katika kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura.

Siku ya Jumapili, wagombeaji wawili wakuu wa urais- Raila Odinga na Ruto- walihudhuria ibada tofauti za kanisa huko Karen na kuwataka wafuasi wao kudumisha utulivu na uvumilivu hata wasiwasi kuhusu kura ukizidi kupamba moto.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved