Wakenya mnamo Jumanne, Agosti 9, walitekeleza wajibu wao wa kiraia kwa kuwapigia kura wagombeaji waliowapendelea kutoka urais hadi wabunge wa bunge la kaunti.
Kaunti zote 47 zilishiriki katika kuchagua seneta wao ajaye.
Baadhi ya wagombea walihifadhi viti vyao huku wengine wakishindwa, kama ilivyo kawaida katika kila uchaguzi
Hii hapa orodha ya Maseneta wateule:
Kaunti ya Migori
Mgombea wa ODM Eddy Oketch alipata kura 295,228, na kushinda kiti hicho.
Kaunti ya Busia
Mgombea wa chama cha NRA Okiya Omtatah alishinda kwa kura 171,681.
Hillary Itela wa ODM aliibuka wa pili kwa kura 59,276.
3. Kaunti ya Homa Bay
Moses Kajwang' wa ODM amehifadhi kiti chake baada ya kupata kura 353,882. Mpinzani wake wa KANU Thomas Ojanga alipata kura 18,690.
Kaunti ya Kisumu
Tom Ojienda wa ODM amejinyakulia kiti hicho kwa kura 413,121. Enos Kudi Okolo wa Jubilee aliibuka wa pili kwa kura 15,575.
Kaunti ya Bungoma
Ford Kenya Moses Wetang'ula amehifadhi kiti chake cha useneta wa Bungoma. Alipata kura 286,143.
Kaunti ya Pokot Magharibi
Mgombea wa chama cha UDA Julius Murgor alishinda kwa kura 72,240.
Kaunti ya Trans Nzoia
Mgombea wa chama cha UDA Allan Chesang amejinyakulia kiti hicho kwa kura 123,793.
Kaunti ya Uasin Gishu
Mgombea wa chama cha UDA Jackson Mandago amejinyakulia kiti hicho kwa kura 252,800.
Kaunti ya Kakamega
Mgombea wa chama cha UDA Boni Khalwale amejinyakulia kiti hicho kwa kura 247,860.
Kaunti ya Bomet
Mgombea wa chama cha UDA Hillary Sigei, amejinyakulia kiti hicho kwa kura 237,192. Enock Kemei wa CCM alipata kura 57,745 huku Weldon Korir akipata kura 41,106.
Kaunti ya Siaya
Mgombea wa chama cha ODM Oburu Odinga amenyakua kiti hicho kwa kura 285,595. Julius Okinda Okinda, mgombea binafsi, aliibuka wa pili kwa kura 33,898.
Tharaka Nithi
Mgombea wa chama cha UDA Mwenda Gataya amejinyakulia kiti hicho kwa kura 71,246. Samwel Ragwa, chama huru alichukua nafasi ya pili kwa kupata kura 46,205.
Kaunti ya Kwale
Issa Boy wa ODM alihifadhi kiti chake baada ya kupata kura 52,772. Katika nafasi ya pili alikuwa Antony Yama wa UDA aliyepata kura 41,762.
Kaunti ya Mombasa
Faki Mwinyihaji amehifadhi kiti chake kwa kutumia tiketi ya ODM baada ya kupata kura 11,040.
Alimwangusha Hamisi Mwaguya wa UDA ambaye alikuwa na kura 76,069.
Kaunti ya Taita Taveta
Jones Mwaruma wa ODM alimshinda mpinzani wake wa karibu, MCA anayeondoka wa Sagala Godwin Kilele wa Jubilee kwa kura 39,142.
Kilele alifanikiwa kupata kura 26,158.
Kaunti ya Narok
Gavana wa sasa Ledama Olekina amefanikiwa kutetea kiti chake baada ya kuzoa kura 135,108.
Alimshinda Gavana Anayeondoka Samuel Tunai aliyepata kura 117,869.
Kaunti ya Makueni
Mbunge wa Makueni anayeondoka Daniel Maanzo wa Wiper ameshinda kwa kura 177,273.
Gavana anayeondoka Kivutha Kibwana aliibuka wa pili kwa kura 59,034.
Kaunti ya Machakos
Agnes Kavindu wa Chama cha Wiper alishinda kinyang’anyiro hicho kwa kura 155,883 dhidi ya Urbanus Ngengele wa UDA aliyeshinda alipata kura 65,603.
Kaunti ya Laikipia
Mgombea wa UDA John Kinyua alitetea kiti chake baada ya kupata kura 59,947.
Kaunti ya Kitui
Seneta wa sasa Enock Wambua amehifadhi kiti chake baada ya kujizolea kura 191,317.
Mgombea huyo wa Wiper alimwangusha Stephen Kilonzo wa UDA, aliyepata kura 49,064.
Kaunti ya Kiambu
Karungo Thang’wa wa UDA ameshinda kiti hicho baada ya kujizolea kura 579,411.
George Maara wa Jubilee aliibuka wa pili kwa kura 112,304.
Kaunti ya Nairobi
Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna ameshinda kiti cha Seneta wa Nairobi baada ya kupata kura 716,876.
Askofu wa UDA Margaret Wanjiru aliibuka wa pili baada ya kupata kura 554, 091.
Kaunti ya Embu
Alexander Mundigi wa Chama cha Democratic aliwashinda wapinzani wake 11 baada ya kupata kura 81, 162.
Gavana wa Embu anayeondoka na mwenyekiti wa Baraza la Magavana Martin Wambora aliibuka wa tano kwa kura 13, 523.
Kaunti ya Nyandarua
Mgombea wa UDA John Methu alipata kura 185,337 dhidi ya seneta anayeondoka Mwangi Githiomi ambaye alikuwa na kura 15,015.
Githiomo alikuwa mgombea Huru baada ya kupoteza uteuzi wa UDA.
Kaunti ya Marsabit
Mgombea wa Chama cha UDA, Mohamed Chute alitangazwa mshindi katika kinyang’anyiro hicho baada ya kupata kura 41,760.
Mgombea wa chama cha KANU Adan Hassan Sheikh Sele alifuata kwa kura 23,206 huku mgombea wa ANC Galgallo Abagaro akipata kura 18,586.
Godana Hargura aliyemaliza muda wake alishika nafasi ya nne kwa kupata kura 18,075.
Kaunti ya Nyamira
Seneta Okong’o Omogeni alihifadhi kiti chake baada ya kupata kura 96,432.
Alimwangusha mpinzani wake wa UDA Mose Nyambega aliyepata kura 43,866.
Adams Mochenwa wa DP alikuwa wa tatu kwa kura 22,235.
Kaunti ya Elgeyo Marakwet
Kipchumba Murkomen alifanikiwa kutetea kiti chake baada ya kupata kura 141,091.
Gavana anayeondoka Alex Tolgos ambaye alikuwa anawania kwa tikiti ya Jubilee alifanikiwa kura 20,648.Kaunti ya SamburuSeneta Steve Lelegwe amehifadhi kiti chake kwa kura 40,066 kwa tiketi ya UDA.
Alimshinda mgombeaji wa ODM Joseph Lepariyo aliyepata kura 2,111 huku Joshua Leparachao wa DAP-K akiwa na kura 485.
Kaunti ya Garissa
Abdulkadir Haji wa Jubilee alinyakua kiti hicho baada ya kupata kura 72,383.
Kaunti ya Baringo
IEBC ilimtangaza William Cheptumo wa UDA kuwa mshindi baada ya kupata kura 141,777.
Seneta anayeondoka Gideon Moi wa KANU aliibuka wa pili kwa kura 71,480.
Kaunti ya Nakuru
Mkurugenzi Mtendaji wa Keroche Breweries Tabitha Karanja alishinda kiti hicho baada ya kupata kura 442,864.
Aliwashinda Koigi Wamwere 6335, Lawrence Karanja 163, Gachinga Mwai 7223, Githenya Mwangi 4680 na John Mututho 36,432.
Kaunti ya Kericho
Aaron Cheruiyot wa UDA amehifadhi kiti chake baada ya kura 292, 295.
Kaunti ya Tana River
Danson Mungatana wa UDA aliwashinda wapinzani wake kumi baada ya kupata kura 34,129.
Mpinzani wake wa karibu Hassan Dukicha (Jubilee) alipata kura 18,082.
Kaunti ya Kirinyaga
Mgombea wa UDA James Kamau Murango alishinda dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Jubilee Daniel Karaba.
Kaunti ya Kilifi
Mgombea wa ODM Stewart Madzayo amehifadhi kiti hicho.
Kaunti ya Lamu
Joseph Githuku ameshinda kiti hicho kwa tiketi ya Jubilee.
Githuku atamrithi Anuar Loitoptip ambaye alishinda kiti hicho kupitia tikiti ya Jubilee mwaka wa 2017.
Kaunti ya Garissa
Abdulkadir Haji wa UDA alichaguliwa tena. Mnamo 2017, alikuwa ameshinda kupitia tikiti ya Jubilee Party.
Kaunti ya Mandera
Gavana anayeondoka Ali Roba wa chama cha United Democratic Movement (UDM) amenyakua kiti hicho baada ya kupiga kura.
Kaunti ya Isiolo
Adan Dulo Fatuma amehifadhi kiti chake.
Alikuwa akiwania kwa kutumia tikiti ya Jubilee.