logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Stori za Ghost: Jamaa ambaye amekuwa akidanganya mpenzi wake mzungu kuwa mkewe ni dadake anaswa

Kwa kuwa mzungu huyo hakuwa tayari kukatiza mahusiano yake na Kyalo alimwagiza wasafiri naye hadi Denmark waishi pamoja kama wanandoa kwa kipindi cha miaka saba kama walivyokuwa wanaishi na mkewe hapa nchini.

image
na Radio Jambo

Makala29 November 2021 - 06:16

Muhtasari


• Kyalo amekuwa akichumbia mzungu kutoka Denmark kwa kipindi cha miaka saba licha ya kuwa ana tayari ana mke hapa Kenya.

•Mzungu yule alimuonyesha Kyalo picha zilizoonyesha akimbusu mke wake na zingine zilizonyesha watoto wake kuthibitisha anafahamu kuhusu ndoa yake.

Ghost studioni

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha 'Stori za Ghost', mtangazaji Ghost Mulee alisimulia kisa kimoja kilichotokea katika eneo la Diani, kaunti ya Kwale ambacho kilihusisha jamaa na mpenzi wake mzungu.

Kulingana na Ghost, jamaa anayejulikana kama Kyalo amekuwa akichumbia mzungu kutoka Denmark kwa kipindi cha miaka saba licha ya kuwa ana tayari ana mke hapa Kenya.

Kwa kuwa mzungu huyo amekuwa akimsaidia  kifedha, Kyalo amekuwa akimdanganya kuwa mke wake ni dadake ili kulinda mahusiano yao.

"Kyalo anachumbia mzungu. Amekuwa akiambia mzungu huyo kuwa mke wake ni dadake kwa miaka saba. Mzungu huyo ambaye anatoka Denmark amekuwa akija kila mwaka na tayari amewajengea kina Kyalo nyumba maanake anajua yule mwanadada ni dadake" Alisimulia Ghost.

"Juzi mzungu huyo  amewashtua baada ya kuja Kenya na kuambia Kyalo kuwa anataka mkutano wa familia. Watu wa familia na wanakijiji wakaitwa. Mzungu kumbe ashafanya uchunguzi wake. Alitoa picha na video  za jamaa wake akamwambia Kyalo kuwa anafahamu amekuwa akimdanganya kwa miaka saba" 

Mzungu yule alimuonyesha Kyalo picha zilizoonyesha akimbusu mke wake na zingine zilizonyesha watoto wake kuthibitisha anafahamu kuhusu ndoa yake.

Kwa kuwa mzungu huyo hakuwa tayari kukatiza mahusiano yake na Kyalo alimwagiza wasafiri naye hadi Denmark waishi pamoja kama wanandoa kwa kipindi cha miaka saba kama walivyokuwa wanaishi na mkewe hapa nchini.

"Sasa hivi Kyallo ameenda Denmark na mzungu na kuacha bibi yake" Ghost alisimulia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved