logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wanasiasa wanawake pia hupata hedhi-Seneta mteule Gloria

Wengi walimuunga mkono huku wengine wakimshambulia vikali kuhusu kitendo hicho

image
na Radio Jambo

Habari17 February 2023 - 10:25

Muhtasari


  • "Ilikuwa niondoke mitandaoni nikashauriwa nisiondoke kwa sababu nimeshaanzisha haya mazungumzo

Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye Seneta mteule Gloria Orwoba ambaye alizungumzia sababu yake kuu ya kutoka kwenye mitandao ya kijamii ya twitter.

Gloria, aliingia seneti tarehe 14 mwezi huu akiwa amevalia nguo zilizo na "damu" hedhi kuteta usambazaji wa sodo za bila malipo kwa mtoto wa kike.

Wengi walimuunga mkono huku wengine wakimshambulia vikali kuhusu kitendo hicho

Gloria alisema kwamba kejeli kwa ajili ya hedhi kwa wanawake inaumiza kwa kila mwanamke.

"Pale bungeni huwezi kuzungumza kabla muda wako hujafika. Nilipoambiwa niondoke niliondoka bila kuzungumza kwa sababu ya sheria za bunge... Unyanyapaa wakati wa hedhi unadhuru. Kuna msichana alijiua kwa sababu ya hili

Kuna mswada tunatengeza wa sodo, miswada huchukua muda kutekelezwa. Nilikuwa nimekaa bunge kwa kama dakika 30 na hakukuwa na tatizo. Nilikuwa sawa mpaka mahali mwanamke mwingine alipoanzisha mazungumzo kuhusu nilivyokuwa

Kejeli kwa ajili ya hedhi kwa wanawake inaumiza kama kitu kingine kile, pia wanasaiasa wa wanawake hupata hedhi,"Alizungumza Gloria.

Huku akizungumzia sula la kutoka kwenye mitandao ya kijamii ya twitter alisema;

"Ilikuwa niondoke mitandaoni nikashauriwa nisiondoke kwa sababu nimeshaanzisha haya mazungumzo. Kilichofanya nitake kuondoka sana ni kuambiwa siwezi kupatiwa uongozi maanake sijui kudhibiti hedhi yangu. Wanaume wakasema pia ni kwa sababu sijapata mwanaume wa kunipa mimba."

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved