logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Sijawahi elewa uhusiano kati ya kipindi cha Patanisho na Waluhya,” - Stephen Letoo

“Sijawahi elewa uhusiano kati ya kipindi cha Patanisho na Waluhya,” Letoo alisema.

image
na Radio Jambo

Makala12 July 2022 - 13:47

Muhtasari


• “Kuwa Mluhya ni kama uchekeshaji. Hakuna mapenzi matamu kama ya kutangazia dunia mzima." mmoja alijibu.

Ripoti wa runinga Stephen Letoo na watangazaji Gidi na Ghost

Ripota maarufu wa runinga humu nchini, Stephen Letoo amezua mjadala mkali kwenye mtandao wa Facebook baada ya kudai kwamba kwa muda mrefu sasa hajawahi kuwa na uelewa kuhusu uhusiano baina ya kipindi maarufu cha redio Jambo alfajiri cha Patanisho na jamii ya Abaluhya humu nchini.

Akiuliza swali hilo kwenye ukurasa wake wa Facebook, nguli huyo mwenye weledi mkubwa katika kushughulikia ripoti za siasa humu nchini kwenye runinga alisema kwamba kipindi hicho kinachoongozwa na manahodha Gidi na Ghost huwa mara nyingi kwa asilimia kubwa wachangiaji na wanaopatanishwa ni watu kutoka jamii hiyo ya upande wa Magharibi mwa Kenya.

“Sijawahi elewa uhusiano kati ya kipindi cha Patanisho na Waluhya,” Letoo alisema.

Katika kipindi hicho kinachoruka hewani kila siku ya wiki kwenye redio Jambo kutoka saa kumi na mbili alfajiri hadi saa nne asubuhi, wengi wanaosikika wakichangia hewani huwa ni Abaluhya na asilimia kubwa ya wanaotaka kupatanishwa mara nyingi huwa ni watu wa jamii hiyo.

“Hakuna kabila nchini Kenya ambalo linachukulia masuala ya ndoa kwa umakini na uzingatifu mkubwa kama kabila la Abaluhya. Watachukua hatua yoyote Madhubuti kuokoa ndoa inayotishia kuvunjika,” aliandika mmoja kwa jina la Leki Muiyia.

Wengine walisema kwamba ni kawaida na wanajamii wa Luhya kupenda redio tangu enzi za idhaa ya taifa ambapo ndio walikuwa wanatawala kipindi cha kutuma salamu redioni huku wengine wakizua utani kuhusu tamko hilo la Letoo.

“Kuwa Mluhya ni kama uchekeshaji. Hakuna mapenzi matamu kama ya kutangazia dunia mzima. Mimi binafsi kipande kinachonifurahisha katika patanisho ni pale mtu anapoambiwa kumwambia mpenzi wake maneno matamu ya mwisho,” mwingine kwa jina la Esmeralda Atenya aliandika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved