Katika kitengo cha Patanisho kwenye Gidi na Ghost asubuhi Radio Jambo, Isaac Ohonjo mwenye umri wa miaka 29 kutoka Butula kaunti ya Busia alitaka kupatanishwa na mkewe Diana Anyango mwenye umri wa miaka 28.
Isaac alisema kwamba waliishi na mkewe katika kipindi cha miaka 3 lakini hawakufanikiwa kupata mtoto.
Alieleza kwamba siku moja alienda kazi na kurudi akapata mkewe aeondoka nyumbani pasi na kumjuisha lolote.
Isaac alisema kwamba mamamkwe wa kambo ndiye alikuja nyumbani na kumhamisha mkewe na alipompigia simu akamwambia kuwa kuna vitu vyake vya saluni alikuwa anapeleka nyumbani lakini hakuwahi rudi kutoka Novemba 2023 hadi sasa.
“Ilikuwa mwaka jana Novemba, nilienda kazi na kurudi nikapata ashaenda…kumuliza alisema kuna vitu alikuwa anataka kupeleka nyumbani ndio akuje… tulikaa kwa ndoa miaka 3 lakii hatukufanikiwa kupata mtoto… tulienda kwa daktari akasema shida iko kwa upande wake na hata wazazi wake wanajua, ni mimi nilikuwa nikimshughulikia…sielewi kwa nini alitoroka…” Isaac alisema.
Akini kwa jinsi Isaac alikuwa anajieleza, watangazaji Gidi na Ghost walihisi kwamba kuna baadhi ya vitu alikuwa anawaficha, kwa sababu alikuwa anashindwa kunyoosha maelezo kwa maswali ambayo walikuwa wanamuuliza kumdadisi ikiwemo kama alikuwa anawajibika kama mume na pia kumshurutisha mkewe kwa tatizo la kutopata mtoto.
Kwa upande wake, Diana Anyango alipopigiwa simu, alishika simu lakini akakata na majaribio mengine ya kumfikia yaligonga mwamba.
Watangazaji walirudi kwa Isaac na baada ya kumdadisi, alifunguka kwamba mama wa kambo wa Diana amekuwa akimshinikiza kuenda nyumbani wafanye mazungumzo kidogo ili kunyoosha mambo na mkewe atarudi.
Isaac alisema kwamba hajafanikiwa kuenda nyumbani kwa kina mke kwa sababu mwezi Desemba amekuwa bize na kazi, akisisitiza kwamba anataka kwanza azungumze na mkewe kabla ya kuenda nyumbani kwani alishamblock.