logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa aagizwa na jamaa mwingine aachane na mkewe, akidai ni mke wake

Njeri alipopigiwa simu alibainisha kwamba hakuna uwezekano wa wao kurudiana huku akidai kwamba mumewe alimdharau.

image
na Samuel Maina

Vipindi15 January 2024 - 06:33

Muhtasari


  • •Bernard alisema mkewe alikasirika alipomuuliza maswali baada ya kugundua anazungumza na jamaa mwingine kwenye Facebaook.
  • •Njeri alipopigiwa simu alibainisha kwamba hakuna uwezekano wa wao kurudiana huku akidai kwamba mumewe alimdharau.

Jamaa aliyejitambulisha kama Bernard Muthike Kariuki ,27, kutoka kaunti ya Kirinyaga alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Ivy Njeri ,22, ambaye alizozana naye mwishoni mwa mwaka jana.

Bernard alisema ndoa yake ya miaka mitano ilianza kuyumba mwezi uliopita kufuatia matatizo ya mawasiliano.

Pia alisema mkewe alikasirika alipomuuliza maswali baada ya kugundua anazungumza na jamaa mwingine kwenye Facebaook.

"Mnamo tarehe 5 Desemba mwaka jana, nilikuwa narudi kazi Isiolo akasema nisimuache nyumbani pekee yake tuendanishe. Nikamwambia ni sawa asubuhi tutatoka pamoja. Baadaye niliporudi kazini, kwa sababu ameweka Facebook yake kwa simu yangu, alienda akafungua Facebook ingine nikapata kuna jamaa wanazungumza naye wakiambiana wapatane," Bernard alisema.

Aliendelea, "Nilipomuuliza, alikasirika. Tulliongea na tukasuluhisha. Baadae akasema amechoka. Nikamuuliza kwa nini. Akasema huwa nashinda nikimkekelesha. Kutoka hiyo siku anasema atakuja na hakuji. Nashangaa kwa nini. Sasa hivi yuko kwao nyumbani. Ako na mtoto wetu. Simjui huyo jamaa ambaye alikuwa akizungumza naye, alisema ni jamaa walikutana Facebook tu lakini hakuwa na noma."

Bernard pia alifunguka kuhusu jambo lingine lililomkera mkewe. Alisema alijaribu kutumia Facebook kumshinikiza Bi Njeri arudi ila mzazi huyo mwenzake hakupenda kitendo cha kumpost kwenye mtandao huo.

"Kutokana na hasira, nilijaribu kuposti kwamba naumia, anasema anakasirika juu ya hiyo. Kuna wakati nilipost picha yake na mimi na watoto, nikasema Njeri rudi nyumbani nakupenda. Nilipost Facebook akasema namuaibisha na mimi nilikuwa najaribu kumrudisha nyumbani," Bernard alisema.

Njeri alipopigiwa simu alibainisha kwamba hakuna uwezekano wa wao kurudiana huku akidai kwamba mumewe alimdharau.

"Haitawezekana. Amekuwa akinifanyia madharau," Njeri alisema.

Pia alipuuzilia mbali madai ya kuzungumza na jamaa mwingine kwenye Facebook.

Bernard alimwambia, "Rudi nyumbani tafadhali. Chochote utakacho nitafanya. Tafadhali rudi. Siwezi kuishi bila wewe."

Njeri hata hivyo alimjibu, "Sikutaki tena. Nilichoka na wewe. Nimefika mwisho. Mimi sitaweza tena." kisha akakata simu."

Bernard aliendelea kufichua masaibu zaidi katika ndoa yake ambapo alifichua kwamba ilikuwa mara ya pili kwa mkewe kum'cheat.

"Wakati moja nikitoka kazini nilpata kuna jamaa alikuwa amesimama mbele yangu akinimbia niachane na bibi yake. Nikashangaa ni mke yake aje na ako kwangu. Hii ilikuwa ni mara ya pili yake kucheat," Bernard alisema.

Je, maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved