logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Nilimchapa mke wangu baada ya kunishuku kuwa na mipango ya kando

“Aliona mdada mwingine alinipigia simu, huyo alikuwa rafiki yangu tuki

image
na Davis Ojiambo

Vipindi04 March 2024 - 05:53

Muhtasari


  • • “Meseji zangu, mke wangu aliona kwa Facebook nikimwambia huyo rafiki yangu kwamba nitakupigia baadae, sasa hivi niko busy." Morris alisema.

Katika Kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kwenye Radio Jambo, kitengo cha Patanisho, kijana kwa jina Morris Evans Awiti kutoka kaunti ya Homabay alitaka kupatanishwa na mkewe Pauline Anyango.

Morris alisema kwamba wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka 4 na watoto wawili lakini walikosana Ijumaa iliyopita kutokana na kile alichokitaja kama ni ‘mambo na mipango ya kando’.

“Aliona mdada mwingine alinipigia simu, huyo alikuwa rafiki yangu tukiwa shuleni. Sasa mke wangu akadhani ni mpango wangu wa kando. Sasa alinipigia kelele halafu nikamchapa na kiboko. Halafu akatoka na kuenda kwa nyanya yake,” Morris alisema.

“Meseji zangu, mke wangu aliona kwa Facebook nikimwambia huyo rafiki yangu kwamba nitakupigia baadae, sasa hivi niko busy. Mke wangu nilimpigia hata leo akasema amenisamehe lakini sijaamini ndio maana nimeleta patanisho,” aliongeza.

Anyango alipopigiwa simu, alipatikana amezima simu.

Morris alisisitiza kwamba licha ya mkewe kumuambia kuwa amemsamehe na anahitaji muda, yeye alikuwa anataka mtoto arudi ili aende shule.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved