logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: "Soda inaisha, pesa hakuna. Credit inaisha, pesa hakuna!" Dada alalamikia wizi wa mdogo wake

"Mimi sipendi watu mkono mrefu. Hana heshima kwa mzazi, unatumia mzazi pesa inamezwa," Bi Mary alilalamika.

image
na Samuel Maina

Vipindi20 May 2024 - 06:21

Muhtasari


  • •Zawadi alisema uhusiano wake na dadake uliharibika mwaka wa 2020 wakati alipopewa kazi ya duka kisha akaiacha.
  • •Zawadi alisema amekuwa akijaribu sana kumuomba radhi dadake ila bado hajapata ujasiri wa kukabiliana naye.

Katika kitengo cha Patanisho, mwanadada aliyejitambulisha kama Sheillah Zawadi ,22, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na dada yake mkubwa Mary Amukoya ambaye alikosana naye takriban miaka minne iliyopita.

Zawadi alisema uhusiano wake na dadake uliharibika mwaka wa 2020 wakati alipopewa kazi ya duka kisha akaiacha.

"Nilikosea sana, sasa najuta tu.  Kuna mwanaume aliniambia atanilea vizuri akaniambia niache hiyo kazi. Nikaacha kazi, nikaingia kwa nyumba, kukaa mwezi moja akawa ananitesa, mahitaji hashughulikii na pia watoto hashughulikii," Zawadi alisimulia.

Aliendelea, "Tuko na huyo mwanaume bado lakini mwaka jana alienda Nairobi. Hadi sasa hajarudi . Aliniacha kwa ploti, lakini sasa niko kwao. Nilifuatilia nikaenda mpaka kwao nikaruhusiwa kujenga. Nikimwambia anisaidie, huwa anasema ningoje mwisho wa mwezi. Mwisho wa mwezi ikifika ananitumia elfu moja pekee. Hiyo ni bajeti ya mahitaji na kuwapeleka watoto shule."

Zawadi alisema amekuwa akijaribu sana kumuomba radhi dadake ila bado hajapata ujasiri wa kukabiliana naye.

"Huwa nafika kwa duka yake alafu narudi nyumbani, huwa naogopa. Niko na watoto wawili, mmoja nilizalia nyumbani," alisema.

Bi Mary alipopigiwa simu, aliweka wazi kwamba mdogo wake anafaa kumtafuta wazungumze ikiwa anataka msamaha.

"Kama ni dadangu anitafute mwenyewe tuongee. Ananijua vizuri, na anajua sina roho mbaya. Mimi sitaki kuongea na yeye kwenye redio. Anitafute. Yeye mwenyewe anitafute. Yeye ndiye anahisi mwenye hatia. Anitafute tuongee," Mary alisema.

Zawadi alisema, "Naogopa sana ata kumfikia. Naogopa, nahisi nimekosea. Alinichapa nikiwa mdogo, lakini sasa sijui...  Nakuomba mama shantel unisamehe kwa niliyofanya. Naskia nimekosea sana. Hata huwa nafika hapo kwa duka nashindwa kuongea na wewe."

Bi Mary alisisitiza kwamba mdogo wake anafaa kupiga hatua ya kumtafuta ikiwa anatazamia kusamehewa.

Aidha, aliendelea kufunguka kuhusu tabia ya wizi ya dadake ambayo ilifanya wakosane.

Dadangu ata ukiweka kitu ya mtoto hapo, atachukua. Ata anaingia kwa wardrobe

"Ata kwa duka, soda inaisha, pesa hakuna. Credit inaisha, pesa hakuna. Anachukua simu ya mzazi, anafuliza. Mzazi akiuliza hasemi chochote. Na sio eti mtu hasaidii watoto wake. Mimi sipendi watu mkono mrefu. Hana heshima kwa mzazi, unatumia mzazi pesa inamezwa," Bi Mary alisema.

Zawadi alidai kwamba tayari amebadilika na akasema kwamba atamtafuta dadake kwa ajili ya kuomba msamaha.

Je, una maoni ama ushauri upi kuhusu Patanisho ya leo?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved