Jamaa aliyejitambulisha kama Suleiman Zuma ,29, kutoka Mombasa alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Mariam Muniafu ,22, ambaye alisema amekuwa akizozana naye mara kwa mara.
Suleiman alisema ndoa yake ya miaka mitatu imekuwa na misukasuko mingi ambayo hawawahi kupata suluhu kamili.
Alisema wasiwasi kuhusu ndoa yake ulizidi baada ya mkewe kutoa pendekezo la wao kutengana.
"Nimekuwa na shida kidogo na mke wangu. Tumekuwa na shida ya kuelewana. Mara nyingi tunakosana. Kila mtu anakuja juu kidogo. Miezi mitatu haiwezi kupita kama hatujazozana. Imekuwa hivyo," Suleiman alisimulia.
Aliongeza, "Juzi jioni baada ya kutoka kazi tukafanya shughuli za kawaida, ilipofika wakati wa kuenda kulala, nikagundua kuna shida na ni kama kuna kitu inamsumbua. Kumuuliza shida ni nini alisema mimi niko complicated amechanganyikiwa hajui nini inamsumbua. Aliniambia anaona hii ndoa yetu ni heri tuende njia tofauti. Alisema hatutakosana lakini ni heri tutengane, mtoto nione kama nitabaki na yeye ama ataenda naye. Hiyo imenikula kichwa siku nzima bado inanisumbua. Alisema anataka aishi kivyake na mimi niishi kivyangu. Mambo ya kuwa bibi na bwana anasema amechoka."
Mirriam alipopigiwa simu alikiri kwamba kumekuwa na misukasuko mingi katika ndoa yao ya miaka michache.
Alidai kwamba mumewe hajakuwa mwaminifu, hata baada ya kuahidi kubadilisha mienendo.
"Tumekuwa tu tukisumbuana, yaani mambo madogo madogo. Huku nyuma alikuwa na wanawake. Alikuwa amesema amebadilika. Mimi nilikuwa nimeamua kwenda njia zangu kwa sababu ni kama namkwaza," Mirriam alisema.
Suleiman alikiri kwamba katika siku za nyuma alikuwa akitaniana na wanawake, tabia ambayo alisema tayari ameacha.
"Hizo vitu ameeleza nilikuwa na matatizo kazini, nilikuwa na marafiki. Lakini nimeacha," alisema Suleiman.
Aliongeza, "Mimi nilikuwa nacheat, lakini nilikuwa nataniana nao. Kweli Nilikuwa nacheat. Nilikuja nikabadilika. Niliona sio vizuri nikabadilika. Kama kuna shida, ni vizuri anieleze ili nijue. Bado ndo tunaanza mahusiano, singependa tukosane. Kweli alikuwa akipata meseji, wakati mwingine simu zinapigwa."
Mirriam alisema, "Kumsamehe nimemsamehe. Nilimsamehe kitambo. Shida ni yeye huwa ananishuku na wanaume. Tukikosana kidogo anasema niende kwa yule mwenye ako sawa."
Suleiman alidai kwamba katika siku za nyuma mkewe aliwahi kumkosea vibaya ila akasema tayari alimsamehe.
Hata hivyo, alimuomba msamaha mkewe na kumsihi akubali waishi pamoja kwa amani.
"Pole kwa yote yenye nilikufanyia. Yote tulikoseana tusahau. Mimi nimebadilika nimekuwa mtu mzuri," alisema Suleiman.
Mirriam pia alikiri kumpenda mumewe na kutaka waendelee kuishi pamoja kwa amani.
Je, una maoni au ushauri upi kuhusu Patanisho ya leo?