'Mungu alipatanisha uhusiano wetu,'Size 8 azungumza baada ya drama yao

Muhtasari

•Mungu alipatanisha uhusiano wetu, ni Mungu wa patanisho size 8 azungumzia uhusiano wake na mumewe

•Wacha Mungu akasifiwe kwa upatanisho wake kupitia mwanawe yesu Kristo

Pamoja:Size 8 na DJ Mo

Kwa siku chache zilizopita familia ya The Muraya's imekuwa kwenye vichwa vya habari baada ya mumewe msanii wa nyimbo za injili Size 8 DJ Mo kusemekana ya kwamba alimdanganya mkewe na kutoka nje ya ndoa.

Mengi yalisemwa huku Size 8 akikiri kuwa alifurahi ya kwamba Mo alijiondoa katika ndoa yao, huku Mo naye akimwambia mkewe kuwa ni wake milele.

Huku akisherehekea ndoa yao, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Size 8 alisema ya kwamba uhusiano wao ulipatanishwa na Mungu ambaye ni Mungu wa patanisho.

 

Huku mashabiki wake wakijibu ujumbe wake wengi waliwashauri wengine wasiweze kuwaamni watu mashuhuri au ukipenda macelebs kwa mambo ambayo wanafanya.

Huu hapa ujumbe wa Size 8;

"Mungu alipatanisha uhusiano wetu kupitia kwake mwanawe yesu kristo mkombozi wetu na ndio juhudi zake mwenyezi Mungu hazibadiliki

Anapatanisha mahusiano kupitia neema ambayo aliimwaga duniani kupitia Yesu Kristo." Aliandika Size 8.

Huku akiendelea na ujumbe wake alisema kuwa Mungu na atukuzwe kwa patanisho yake na uzuri wake.

"Tazama uweza wa Mungu wa upatanisho ulioonyeshwa kwa ulimwengu kuona,wacha jina lake Mungu likasifiwe, nisaidieni kumsifu Mungu wa patanisho."