Orodha ya wanahabari mashuhuri ambao wanatazamia kujiunga na siasa

Muhtasari

•Wanahabari hao kweli wataweza katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti

•Siasa inawafaa ama wanapaswa kufanya kazi yao ya uhanahabari

•Orodha ya wanahabari maalum waotazamia kujiunga na siasa

Betty 1
Betty 1

Kuwa mwanasiasa si jambo rahisi kwa maana unahitaji elimu jinsi ya kuzungumza na wananchi endapo unatafuta kura kwao.

Ni wengi ambao huwa wanatazamia  kuwa wanasiasa lakini kwa uoga wao wanazima ndoto yao na kuendelea na mambo yao huku wakiwa na hofu ya kuanza safari ya kujipigia kampeni.

Si mmoja au wawili bali baadh8 ya wanahabari tajika na maalum wametangaza azmio yao ya kuwa wanasiasa katika siku za usoni na hii hapa orodha ya wanahabari ambao wapaswa kuwafahamu ambao wana maazimio ya kuwa wanasiasa.

1.Betty Kyallo

Aliyekuwa mwanahabari wa runinga ya K24, huku akiwa katika mahojiano alifichua kuwa anampango wa kujiunga na siasa.

Betty-Kyallo-smiling- 1
Betty-Kyallo-smiling- 1

Hata hivyo Betty hakufichua atawania kiti kipi na katika kaunti ipi.

2. Jalang'o

Baada ya kuzindua runinga yake na kuandika na kampuni ya Radio Africa Group, alisema kuwa kazi ya utangazaji katika redio ya Kiss ndio ya mwisho huku akitakka kujiunga na siasa.

3.Jacque Maribe

Aliyekuwa mwanahabari wa runinga ya Citizen Maribe alisema kuwa kama ni kuwania kiti atawania katika kaunti yake ya Murang'a, kuwa mwakilishi wa wanawake huku akidai kuwa wanawake pia wamemuomba kujiunga na siasa.

7bbb6c1d-cad8-447e-b913-2df8b7c5c842_0
7bbb6c1d-cad8-447e-b913-2df8b7c5c842_0

4.Andrew Kibe

Aliyekuwa mtangazaji wa redio ya Kiss, hivi majuzi alisema ya kwamba atajiunga na siasa huku wakenya wengi wakimkosoa na kumwambia anapaswa kufanya kazi yake ambaye ni ya utangazaji.

64579648_174247060261854_1394014274228126795_n
64579648_174247060261854_1394014274228126795_n

Lakini je watajiunga na siasa au ni porojo tu, na kama watajiunga kwa kweli watawezana na kampeni na kinyang'anyiro chaa uchaguzi huo?