'Mimi ni mzuri kwa kupokea watu,'Hamisa azungumzia kurudisha uhusiano na Zari

Muhtasari
  • Nina matumaini tupatane ili watoto wajuene kwa maana ni wa baba mmoja
  • Mimi ni mtu ambaye huwaga mzuri sana kwa kupokea watu
  • Tuna matumaini huko mbele kutakuwa sawa licha ya changamoto ambazo tunapitia
HAMISA-MOBETTO
HAMISA-MOBETTO

Hamisa Mobetto ambaye ni baby mama wake staa wa bongo Diamond ameweka mambo wazi huku akisema yuko tayari kupatana na Zari Hassan na kurudisha uhusiano wao.

Akiwa kwenye mahojiano Hamisa alisema kuwa ni mzuri kwa kuwapokea watu na yuko tayari kuweka amani kati yake na Zari kama vile yuko na uhusiano na aliyekuwa mpenzi wake Diamond Tanasha Donna na Wema Sepetu.

Alipouliza kama kuna siku itakaja tokea wawili hao wawe marafiki alisema kuwa,

 

"Kama itakuja kutokea, mimi I’m here. Mimi ni mtu ambaye huwaga ni mzuri sana kwenye kupokea watu, na mkarimu. Kwa hiyo kama imepangwa, kama itakuja kutokea sawa I’ll be here.” Alizungumza Hamisa.

Hamisa alipoulizwa kama baby mama wa staa wa bongo Diamond wamepanga au watapanga wawakutanishe watoto wao ili wajueni mama huyo alisema anamatumaini kuwa yatatendeka.

zari
zari

“When it comes to kids ambao wana baba mmoja kila mtu anahope familia zikutane vitu viwe vimoja, kila mtu awe ni kitu kimoja tuzidi kusogesha mbele kwa hiyo kama kuna any circumstances ama shida, we are hoping huko mbeleni kuwe sawa."

Mbali na kuwa rafikiye Wema na Tanasha bado ugomvi upo kati yake na Zari Hassan ambaye ana watoto wawili wa Diamond.