Msanii Sudi boy yuko katika maombolezi baada ya kumpoteza mmoja wa mpendwa wake

Muhtasari
  • Msanii Sudi hataweza kutoa kibao chake kilichokuwa kimesubiriwa sana
  • Anaomboleza kifo cha binamu yake, huku akiwaomba mashabiki msamaha
  • Sudi atatangaza ni lini ataweza kutoa kibao chake kipya
sudiboycover
sudiboycover

Msanii tajika wa humu nchini Sudi Mohammed almaarufu Sudi Boy yuko katika maombolezi baada ya kumpoteza binamu yake.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya instagram Sudi aliwaomba mashabiki wake msamaha na kusema kwamba hataweza kutoa kibao chake ambacho kilikuwa kimesubiriwa sana siku ya ijumaa kwa maana wamempoteza binamu wake.

Msanii huyo alisema kuwa atasema ni siku gani ambayo atatoa kibao hicho.

 

"Mambo vipi watu wangu mtaniwia radhi leo sito weza kuachia ngoma kwasababu tumepatwa na msiba wa cousin yangu kwajina rehema kingi kaaga dunia jana kwahiyo inshallah nta wapa update siku ya kuachia ngoma R.I.P rehema kingiInna lillahi wainna ileihi rajiun." Aliandika Sudi.

Mashabiki wake walimuelewa na kisha wakatuma jumbe za risala za rambi rambi na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

selectressgithiro: Pole kwa msiba🙏🙏,mungu awe na wewe pamoja na familia yenu

lizz_jahsolja: Poleni may her soul rest in peace

fahmisalminInna:  lilahi wa inna ileihi rajiuun

moudy2152 :Innallilahi wainaillah rajiun

djjr254:  Pole Sana My Brother, Jipe Nguvu, Itakua Sawa 🙏🏼

 

nemanja_al_farsi : Pole buddy

djdeklack :Pole kwa msiba bro

arniedice: Pole kaka kwa msiba🙏ngoma tunaitegea brah 🔥🔥