'Labda kuna ndoa kamili huku nje lakini yetu si kamili,' DJ Mo asema

Muhtasari
  • Kunaweza kuwa na ndoa kamili humu nje lakini yetu si kamili DJ Mo azungumza
  • Sisi sin kamili na hatutawahi kuwa kamili, huwa tunapigana na kupitia mambo amabyo kila mmoja hupitia
  • Jambo moja ambalo ni la kweli tunapendana sana na Mungu yuko katikati
Dj Mo na Size 8
Image: Hisani

Mcheza deki DJ Mo na mkewe msanii wa nyimbo za injili Size 8 wiki chache zilizopita wamekuwa kwenye vichwa vya habari hii ni baada ya madai kuibuka kuwa Mo alienda nje ya ndoa.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagrama Mo alisema ya kwamba kunaweza kuwa kuna ndoa kamili humu je lakini yake si kamili.

"Japo kuwa ..labda kuna ndoa kamili humu jje lakini yetu si kamili, tutakuwa tukiwadanganya kuwa hatuna panda shuka katika ndoa yetu

 

huwa tunapigana kama kila mmoja wenu, huwa tunapitia mambo ambayo kila mmoja wenu anapitia." Aliandika Mo.

Huku akiendelea kunakili ujumbe wake alisema ya kwmba wao si kamili kama vile wengi wanadhani na hawatawahi kuwa kamili.

"Sisi si kamili na hatutawahi kuwa kamili kile unaona ndicho utakachopata, lakini jambo moja la ukweli tunapendana sana na Mungu yuko katikati."

DJ Mo aliandika haya huku akiwa ameposti video ya mkewe Size 8 akiogelea.