Wacheshi waomba wasamaria wema kuwasaidia kuchanga milioni 1 kugharamia mazishi ya Othuol

Muhtasari
  • Mchekeshaji Othuol aliaga jumapili iliyopita huku mazishi yake yakipangwa ya jumamosi,24
  • Wacheshi wawaomba wasamaria wema kuwasaidia kuchanga millioni moja
Kibonzo cha Marehemu Othuol Othuol

Tasnia ya ucheshi inawaomba wasamaria wema ili waweze kuwasaidia kuchanga milioni moja ya kugharamia mazishi yake mwendazake Othuol Othuol.

Othuol aliaga dunia jumapili iliyopita huku mengi yakisemwa kuwa tasnia hiyo ilimuachilia alipokuwa anataka usaidizi wao.

Othuol ambaye jina lake kamili ni Maurice Onyango Ben aliaga baada ya kuugua uvimbe wa akili, na atazikwa nyumbani kwao Jumamosi ya tarehe 24.

 
 

Ijumaa,16 Oktober wacheshi hao waliweka harambee ya kumchangia mwendazake ambapo wacheshi walijitokeza.

Huku akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa wacheshi nchini Ken Waudo alitupilia mbali madai ya kwamba walimtenga Othuol alipokuwa anahitaji usaidizi wao huu hapa usemi wake;

"Uvumi ambao unaenea sana kwenye mitandao ya kijamii kuwa Othuol alikuwa anatuma jumbe akitaka usaidizi ni uongo na jambo ambalo si nzuri

kwa vikundi ambavyo tulikuwa hamna siku moja ambayo Othuol alisema ana shida tukakosa kumsaidia tulichanga elfu mia moja kwa mara ya kwanza ambapo alitibiwa nazo na kurudi nyumbani

Hata alivyotuma jumbe akihitaji chakula na pesa tulimsaidia, alikuwa anatumia watu kadhaa ujumbe huo tulisimama na Othuo kabla ya kifo chake

tulikuwa tayri tumechanga shillingi elfu 137,000." Aliongea Waudo.