Tuache ulevi kupindukia ni pombe,'Muigizaji Silprosa awashauri wasanii

Muhtasari
  • Silprosa awashauri wasanii kuwa wenye kuajibikia maisha yao 
  • Alisema marehemu Othuol Othuol alikuwa anabugia mvinyo sana
  • Marehumu Othuol alipatikana na maradhi ya kifua kikuu mwaka wa 2019
Othuol-34-1-1
othuol othuol Othuol-34-1-1
Image: hisani

Muigizaji wa kipindi cha Auntie Boss Sandra Dacha anayefahamika kama Silprosa amefichua mambo kadhaa kuhusu mwendazake mcheshi Othuol Othuol huku akiwashauri wasanii wapunguze uraibu wa pombe na waajibikie maisha yao.

Silprosa amekuwa rafiki wa karibu Othuol kabla ya kifo chake, muigizaji huyo ni miongoni mwa wanakamati wanaongoza mazishi ya mwendazake ambayo yameratibiwa kufanyika Jumamosi tarehe 24 Oktoba.

Othuol aliaga dunia wiki jana siku ta Jumapili.

 

 
 

Akiwa kwenye mahojiano siku ya Ijumaa, Silprosa alisema kuwa Othuol alikuwa anabugia pombe sana hali iliyomsababishia maradhi ya ini na kutibiwa.

"Othuol alikuwa anabugia pombe sana, miaka minne iliyopita alipatikana na matatizo ini, mwaka wa 2019 Februari alipatikana na ugonjwa wa kifua kikuu. Alitibiwa na kupewa dawa na hakumaliza dawa zenyewe," Alisema Silprosa.

Aliongeza kwamba,

"Ni kama alikuwa amechoka na kutojali maisha yake,wasanii tuacheni pombe na tuwe wenye kuajibika".

Pia alisema kwamba pesa ambazo zinachangwa si za kugharamia mazishi tu pekee bali za kuwapa familia yake ambayo ilikuwa inamtegemea.

(Mhariri Davis Ojiambo)