Mnaharibu nguvu zenyu bure-Anerlisa Muigai kwa wanaume wanaomfanyia haya

anerlisaposing
anerlisaposing

Anerlisa Muigai amewaonya wanaume ambao wanamfuata na kutomfuata kila mara kwenye mitandao ya kijamii huku akiwaambia kuwa wanaharibu nguvu za bure na hamna kitu kizuri ambacho kitawatendekea kutoka kwake baada ya kufanya hayo.

"Kwa wanaume amabo mnanifuata na kisha mnaacha kuniata na tena mnanifuata tena kama mara 10,000 kwenye mitandao ya kijamii ili kupata mawazo yangu au kunipata

Tafadhali kateni huo ujinga, mnaharibu nguvu zenyu." Muigai Aliandika.

Haya yanajiri siku chache baada ya uvumi kuenea kuwa wameachana na mumewe Benard Paulo almaarufu Ben pol.

Kuachana kwao hawakuweza kukupeleka hadharani, huku akizungumzia kuachana kwao alisema kwamba anapenda kupewa heshima yake na kulinda heshima yake hadharani.

Huku akisimulia kisa kimoja alipopokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu na kumuuliza iwapo anajua kile mume wake alichokuwa anafanya kwenye mitandao ya kijamii ya instagram.

"Mtu alinipigia simu na kuniuliza kama nafahamu kile mume angu alichokuwa anafanya kwa maana alikuwa anasema mambo ambayo hakuelewa alinitumia mpaka picha

Kwa bahati mbaya sikuweza kutazama, lakini kuweka mambo wazi hatuyuko katika hali nzuri mimi ni mtu ambaye napenda kulinda heshima yangu, na kile najua ni kwamba napenda kupewa heshima, na wanaume wote wanapaswa kufanya hivyo kwa wake zao."