Mchekeshaji Churchill yaonekana amechoshwa na sarakasi za baadhi ya wasanii ambao aliwapa fursa katika jukwaa lake wajijenge lakini wakati wote wamekuwa wakitoa cheche za maneno na shutuma wakati wanapopatikana mashakani .
Wakati wa mazishi ya mchekeshaji Othuol Othuol Churchill aliamua kusema yote moyoni kwa kumtaka Jalangó kutafsiri hotuba yake .
Churchill aliwataka wachekeshaji wenzake kujijenga na kukoma tabia ya kenda katika mitandao ya kijamii kuwaambia mashabiki wao kila jambo linalofanyika katika maisha yao .
‘Acheni kuwaita mashabiki wenu familia …wakati utakaposhindwa kuwachekesha basi hutakuwa tena familia . Acha kuamka kila siku na kuwaambia kuhusu ulichokula ,ulivyovalia..acheni!’alisema Churchill
Zeddy ambaye amekuwa chini ya Churchill katika fani ya ucheshi amekuwa akigonga vichwa vya habari kwa msimamo wake wa kueleza masaibu wanayopitia wachekeshaji wenzake . Amekuwa akisema kwamba wengi wao wana matatizo ya fikra kwa sababu ya shinikizo inayoambatana na kazi yao ya kuangaziwa katika runinga na vyombo vya habari .
Wakati Churchill alipokuwa akizungumza na wenzake katika fani ya burudani alimgeukia Zeddy na kumuambia
" Unaniskia Zeddy? Achana na wanablogi ,wanapata pesa kupitia stories zako .Jikuuze pamoja na brandi yako na pesa zitakufuata’