'Tutakuja mazishi yako kama road trip kuona kama ulijenga,'Ushauri wake Mejja

Muhtasari
  • Rappa Mejja awashauri wanaopuuza familia zao, huku akiwaambia wanapaswa kushilia familia zao kwa maana ni muhimu
Mejja
Image: Hisani

Rappa Mejja ni msanii ambaye anapendwa sana wa sanii wenake na hata mashabiki kwa moyo wake mnyenyekevu kwa kila jambo.

Awali msanii huyo amekuwa akitoa vibao baada ya vingine huku vikipendwa sana na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii ya youtube.

Wiki jana Mejja alikana madai kuwa ailipwa pesa ili aweze kufanyiwa mahojiano na kukosa kujitokeza huku akisema kuwa atachukua likizo katika kazi yakke kwa maana anapenda amani yake.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram mejja amewashauri wanaume au wanawake ambao wanakataa familia zao na kujipenda tu pekeyao.

Familia ni muhimu sana na haipaswi kupuuzwa kwa lolote lile, jamaa zako ndio tu watasimama nawe kwa kila mapito ya familia.

Awali hasa wakati huu wa janga la corona kumekuwa na kesi nyingi ambazo watu wengi wanapuuza familia zao na kuwaacha watoto wake.

Mejja aliona hayo si mema na alikuwa na haya ya kuwaambia ambao wana tabia kama ile,

"Nitazidi kuwaambia tenga muda wa familia yako, hao ndio watakuzika sisi marafiki zako tutakuja mazishi yako kama road trip kuona kama ulijenga kwenu ama ni raha ilikuwa inakumaliza 

Shikilia familia muhimu." Mejja aliandika.

Swali kuu ni je wewe unatambua familia yako liha ya mambo yote ambayi mmepitia? ama ukipata umesahau kuwa una familia.