'Hii mapenzi ya mitandaoni utapata nyumbani ni vita,'Mashabiki wamwambia Bahati na Diana Marua

Muhtasari
  • Diana Marua na mumewe Bahati wapokea kejeli kutoka kwa mashabiki
dm
dm

Kwa muda sasa msanii Kevin Bahati na mkewe Diana Marua wamekuwa wakipakia picha si haba kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya mashabiki wakiwapongeza na wengine wakiwakejeli.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya instagram Bahati aliposti picha na kuandika ujumbe kuwa yeye na mkewe hawakosani ilhali kunamsemo unaosema wakosanao ndio wapendanao.

"Wanasema Wakosanao Ndio Wapendanao... Sisi Hatukosanangi Aki Nabado Tunapendana 😆 ARE WE OKEY???" Bahati Aliandika.

Wakati huo Diana aliposti picha hiyo kwenye ukurasa wake huku akipokea kejeli kutoka kwa mashabiki.

Baadhi yao walimwambia kuwa upendo ambao wanawaonyesha mashabiki kwenye mitandao ya kijamii utapata kuwa nyumbani hamna upendo huo.

Huku wengi walisem kwamba wawili hao wamezidi na kujigamba kwenye mitandao hiyo.

Hizi hapa baadhi ya hisia za wanamitandao;

Gracie Grace: Hii mapenzi ya social media utapata hta sio ya ukweli kwanyumba 😂😂.. ogopa soshomedia

Ruphy Michael: Nikiwa mkubwaa nataka kuwa kama nyinyi

Heis Nuby: na baha ni mdogo kweli anaonewaaa😢

 
 

Wanjiru Cate: Tunajua mnapendana si muache hii kushoiinda kupost... mmezidi sasa pia nyinyi