'Ndio niliavya mimba ya Msizwa,'Dada yake Diamond Platnumz akiri

Muhtasari
  • Esma adai kwamba pesa ni kila kitu kwake na si uhusiano wa kimapenzi
  • Pia alifichua kwamba aliavya mimba ya Msizwa kwa maana hakuwa anampenda
  • ESma alisema kwamba hajawahi temwa na mwanamume yeyote bali ni yeye huwa anawatema

Kupitia kenye ukurasa wa instagram dada yake staa wa bongo Diamond Platnumz,Esma Platnumz alikiri kwamba aliavya mimba ya aliyekuwa mumewe bwana Msizwa.

Kulingana na Esma aliavya mimba hiyo kwa sababu hakuwa anampenda mumewe na bado walikuwa wameachana wiki moja baada ya kufunga pingu za maisha.

NI harusi ambayo ilihidhuriwa na wasanii tofauti.

 

Baada ya miezi mitatu wawili hao walitemana, jumapili Esma aliwaacha wanamitandao midomo wazi baada ya kufichua ambayo wengi hawakuwa wamefahamu.

"Nataka kuwajibu wote ambao wanasema kwamba niliavya mimba,ni ukweli, ndio nilifanya hivyo kwa maana siwezi zaa mtoto na kutumaini kumlea na mwanamume ambaye sina hisia zake

KItu ambacho najaribu kusema ni kwamba kama ningemzaa mtoto huyo singempenda, unahitaji kuzaa mtoto na mtu ambaye unampenda 

Kwanini umlete mtoto duniani lakini mwishowe unamchukia." Esma Alifichua.

Huku akizungumzia kuhusu uhusiano wao au ndoa yao alisema,

"Watu wacheni kunishambulia ukweli kwamba  niliavya mimba, nilimuoa ili kujifurahisha katika maisha ya utajiri

Baada ya muda mfupi wiki moja hivi tulikuwa tumeachana, nilijaribu kukaa naye kwa miezi,tulikubaliana kuingia kwa ndoa lakini baada ya muda mfupi tuachane na kila mtu aende kwa njia yake

 

Kwa hivyo sikuwa naye kwa ajili ya mapenzi na sikuwa nataka mtoto ata."

Pia mwanabiashara huyo alisema kwamba hajawahi achwa na mwanamume yeyote bali ni yeye huwa anawatema.

Esma alisema kwamba pesa ndio kila kitu katika maisha yake na wala si uhusiano wa kimapenzi.