Orodha ya wakenya mashuhuri waliotafuta kiki mwaka wa 2020

Muhtasari
  • Wakenya mashuhuri waliotafuta kiki mwaka wa 2020 kupitia kwenye mitandao ya kijamii
Shakilla
Image: Hisani

Kutafuta kiki kwenye mitando ya kijamii kwa baadhi ya watu mashuhuri ni jambo ambalo wanaweza kufanya kwa kufumba na kufumbua.

Kuna baadhi ya wakenya mashuhuri ambao walipata umakini wa wakenya baada ya kutafuta kiki kwa njia tofauti.

Wengi tuliwashuhudiwa na kuwaona baada ya kutafuta kiki mwaka wa 2020.

 

Hii hapa orodha ya wasanii,wacheshi na wakenya mashuhuri waliotafuta kiki ili kuendeleza usanii wao.

1.Size 8 na DJ Mo

Wawili hao wlivuma kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya burudani baada ya madai kwamba DJ Mo alikuwa na mpenzi mwingine nje ya ndoa.

Wawili hao walizidi kuonyesha mashabiki mapenzi yao yamenoga licha ya madai hayo.

Baada ya madai hayo mashabiki walidai kwamba wawili hao walikuwa wanatafuta tu kiki.

Baada ya muda mfupi Size 8 walitoa kibao huku akimshirikisha msanii wa Tanzania Rose Muhando.

2.Diana Marua na Bahati

 

Wawili hao waliacha kufuatana kwenye mitandao ya kijamii huku Diana akifuta picha zake na Bahati kwenye ukursa wake wa instagram.

Wawili hao walijifanya wameachana bali walikuwa wanatafuta kiki ili kuendeleza kibao chao ambacho kinafahamika kama 'Mtaachana tu'.

3.Eric Omondi

Mchekeshaji huyo anafahamika sana kwa ucheshi wake, huku akianza kipindi kinachofahamika kama 'Wife material'. huku akiwaambia mashabiki kwamba anatafuta bibi.

Eric alifanya vyovyote vile ili wanamitandao waamini kwamba anatafuta bibi.

Hii leo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alifichua kwamba  kipindi hicho kilikuwa kimeandikwa tu na cha kuburisha.

4.Shakilla

Alifahamika baada ya kufichua wanaume ambao amefanya ngono na wao huku mwishowe akiomba msamaha.

Mwanasosholaiti huyo chipukizi amekuwa akifanya chochote kile ili avume kwenye mitandao ya kijamii.