Hawa niwafanyie nini?DJ Mo asema haya kuhusu wanawe

Muhtasari
  • Je umewahi patana na DJ Mo akiwa mchofu asubuhi, ni kwa ajili hapati usingizi wa kutosha kwa ajili ya watoto wake
SIZE.8 (1)
SIZE.8 (1)

Mcheza Santuri DJ Mo ni baba wa watoto wawili na mume wa mke mmoja msanii wa nyimbo za injili Size 8.

Ni familia ambayo imekuwa na umoja licha ya changamoto ambazo wawili hao wamekuwa wakipitia.

Mwaka jana DJ Mo na mkewe walikuwa kwenye vichwa vya habari baada ya madai tofauti ya udanganyifu.

Muraya-ladasha-size-8-mpasho
Muraya-ladasha-size-8-mpasho
 

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Mo alipakia video ya watoto wake wakiwa wamelala kwenye kitanda cha wazazi wao.

Mo alisema kiini kimoja cha kuwa amechoka asubuhi na mapema ni kwa ajili hapati usingizi mwema kwa sababu ya wanawe ambao hawajali maslahi yake na mkewe.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook Mo akitoa maoni kuhusu video hiyo alisema wawili hao hawalipi gharama ya nyumbani ilhali wana lala kama wao ndio wenyeji.

"Hawa niwafanyie nini πŸ€£πŸ™†β€β™‚οΈ, hii ndio sababu kuu ya kupatana na mimi nikiwa nimechoka asubuhiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚... kila mmoja ana chumba chake cha kulala lakini wawili hawa katikati ya usiku wanakuja kitandani kwetu πŸ™†β€β™‚οΈ. Sasa mimi na mke wangu @size8reborn nimaskwotaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kwa bed yetu..@muraya.jnr hajali ataa πŸ˜‚ @ladashabelle.wambo sina maneno kwako." Aliandika DJ Mo.

Licha ya kejeli ambazo wamepokea, wamethibitisha kwamba upendo wao hauwezi tenganishwa na mwanadamu yeyote.