Siamini maisha ya ndoa, kwa maana nilipitia dhuluma za kijinsia-Karen Nyamu

Muhtasari
  • Karen Nyamu afichua kunawakati alidhulumiwa na aliyekuwa mumewe

Mwanasiasa Karen Nyamu akiwa kwenye mahojiano na radiojambo alisema kwamba hana imani yeyote katika ndoa hii ni baada ya kudhulumiwa kijinsia awali akiwa kwenye ndoa.

Nyamu ambaye alidaiwa kuwa na uhusiano na mwanamuziki Samidoh alisema kwamba alikuwa kwenye ndoa ambapo mumewe alimdhulumu na hakutaka azungumze naye.

"Napenda watoto, na ninapenda watoto wangu lakini siamini ndoa kwa maana nikiwa na mia ishirini nilidhulumiwa na aliyekuwa mume wangu

 

Sikuripoti kwa polisi kwa maana alikuwa mwanasiasa wakati huo, nilikuwa nafanya kazi kwa kampuni yake

Alihisi kuwa anaweza niambia kila kitu, lakini wakati huo hakujue hangeweza kunielekeza au 'kunicontrol'

Nina akili na mawazo kuwa naweza jisimamia kwa kila kitu, pia nilihisi nikienda kuripoti kwa kweli hamna kitu ingetendeka kwa maana alikuwa mtu ambaye alikuwa anajulikana sana." Aliongea Karen.

Karen ambaye aliwania kiti cha mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Nairobi mwaka wa 2017, alipoulizwa kwanini hakutoka katika ndoa hiyo mapema alisema kwamba mwanasias huyo alikuwa anamtishia maisha.