Nimeokoka sijawahi kubugia vileo-Abel Amunga aweka mambo wazi

Abel Amunga
Image: Radiojambo

Muigizaji Abel Amunga akiwa kwenye mahojiano na radiojambo alifichua kwamba kadha wa kadha kuhusu maisha yake ya uigizaji.

Abel alifichua kwamba katika uigizaji mwingi uonekana akiwa ana bugia vileo hasa kwenye kipindi cha selina ambacho hupeperushwa katika runinga ya maisha magic.

Pia alisema licha ya kuwa uigizaji umekuwa mzuri kwa upande wake kuna baadhi ya changamoto ambazo hupitia katika kazi yake.

 

"Nafurahia sana kazi yangu, lakini kunakipindi ambacho watu wanatarajia uwe kama mwakilishi wadi, endapo wanahitaji msaada wanakuja kwako ukikosa kuwasaidia wanaona wewe ni mkono ghamu.

IMG-20200723-WA0080(1)(1)
IMG-20200723-WA0080(1)(1)

Kuna wale wanaona ukiigiza katika televisheni nikiwa na pombe, lakini ukweli ni kuwa sjawahi kunywa pombe wananiukumu na uigiaji wangu." Alisema Amunga.

Huku akizungumzia maisha yake ya ndoa alikuwa na haya ya kusema,

"Tangu mama yake Ruth aage unia sijawahi oa, aliacha Ruth akiwa na miaka 7 sitaki huapa kwamba sitoa tena lakini Mungu akileta mwanamke mzuri nitaoa."